Mwananchi Digital
GAMBO AIBUKIA KANISANI
- Title
- GAMBO AIBUKIA KANISANI
- Runtime
- 5:26
- Date posted
- 17 days ago
- Description
- Arusha. Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini na Mkuu wa zamani wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, ameibuka hadharani baada ya kipindi kirefu cha ukimya wa kisiasa, akiwashukuru wananchi wa Arusha kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chake cha miaka mitano ya ubunge.
Gambo alitoa kauli hiyo Juni 21, 2026, alipokuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Makao Makuu ya Kanisa la Pentecostal Revival Church (PRC) Kanda ya Kaskazini iliyofanyika jijini Arusha.
Katika hotuba yake, Gambo pia amezungumzia umuhimu wa haki katika kujenga amani ya kudumu nchini akisema kuwa haiwezi kutenganishwa na haki.
- Title
- CHARLES ABEL: HIKI NDICHO KILICHOIPONZA YANGA KIPIGO CHA AZAM CHA MABAO 3-2, IKIAGA FA
- Runtime
- 10:00
- Date posted
- 18 days ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- WAZIRI MKUU WA UINGEREZA AJIUZULU RASMI, AACHIA UONGOZI LABOUR
- Runtime
- 1:09
- Date posted
- 18 days ago
- Description
- Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Uwaziri Mkuu pamoja na uongozi wa Chama cha Labour, katika hatua inayotajwa kuashiria mabadiliko makubwa ya kisiasa nchini humo.
Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu Juni 22, 2026, imeelezwa kuwa Starmer ameamua kuachia madaraka kutokana shinikizo la kisiasa lililokuwa likiongezeka ndani ya chama chake pamoja na mijadala ya ndani kuhusu mustakabali wa uongozi wa serikali.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uamuzi huo umefungua rasmi ukurasa mpya ndani ya Chama cha Labour, huku mchakato wa kumpata mrithi wake ukitarajiwa kuanza mara moja.
Hata hivyo, Ofisi ya Waziri Mkuu imeeleza kuwa taratibu za mpito wa madaraka zitaendelea kwa utaratibu ili kuhakikisha hakuna pengo la uongozi katika kipindi hiki cha mabadiliko.
Endelea kufuatilia Mwananchi..
- Title
- HATARI KUBWA UKRAINE, RUSSIA YAZINGIRA MJI MUHIMU
- Runtime
- 3:49
- Date posted
- 18 days ago
- Description
- Ukraine. Mji wa Kostyantynivka ulioko mashariki mwa Ukraine, unakabiliwa na tishio kubwa baada ya vikosi vya Russia kuendelea kusonga mbele, na kuingia ndani ya maeneo ya mji huo huku vikijaribu kuuzingira kutoka pande mbalimbali, Wanajeshi wa Ukraine walioko mstari wa mbele wanasema hali katika eneo hilo imekuwa ngumu zaidi, ingawa viongozi wa kijeshi wa Ukraine bado wanasisitiza kuwa mji huo haujaanguka mikononi, mwa adui.
Kostyantynivka inachukuliwa kuwa lango muhimu kuelekea maeneo mengine ya Donbas, ikiwa Russia itafanikiwa kuudhibiti mji huo, itapata nafasi ya kusonga mbele kuelekea miji ya Kramatorsk na Sloviansk, ambayo ni ngome kuu zilizobaki chini ya Ukraine katika mashariki mwa nchi hiyo, kukamatwa kwa mji huo kutakuwa hatua muhimu kwa Moscow katika kufanikisha lengo lake, la kuiteka Donbas.
Kwa mujibu wa wanajeshi wa Ukraine waliolizungumza suala hilo kwa masharti ya kutotajwa majina, wanajeshi wa Russia wamekuwa wakiingia katika maeneo ya nyuma, k...
- Title
- KINACHOENDELEA MUDA HUU UWANJA WA CCM KIRUMBA | YANGA, AZAM NANI KUIFUATA SIMBA?
- Runtime
- 4:17
- Date posted
- 19 days ago
- Description
- Hali ilivyo nje ya Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza muda mfupi kabla ya kuanza kwa mechi ya nusu ya Kombe la CRDB kupigwa kati ya Yanga dhidi ya Azam, leo, Juni 21, 2026.
- Title
- MSUVA: NILITAMANI TUCHEZE KOMBE LA DUNIA KAMA CONGO YA FISTON MAYELE
- Runtime
- 14:52
- Date posted
- 19 days ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- #live RAIS SAMIA AKIMPOKEA RAIS NETUMBO NANDI-NDAITWAH, IKULU DAR ES SALAAM JUNI 20, 2026
- Runtime
- 23:27
- Date posted
- 19 days ago
- Description
- #live RAIS SAMIA AKIMPOKEA RAIS NETUMBO NANDI-NDAITWAH, IKULU DAR ES SALAAM JUNI 20, 2026
- Title
- #live RAIS SAMIA AKIMPOKEA RAIS NETUMBO NANDI-NDAITWAH, IKULU DAR ES SALAAM JUNI 20, 2026
- Runtime
- 34:24
- Date posted
- 19 days ago
- Description
- #live RAIS SAMIA AKIMPOKEA RAIS NETUMBO NANDI-NDAITWAH, IKULU DAR ES SALAAM JUNI 20, 2026
- Title
- SITA WAFARIKI AJALI YA BASI NA LORI KAHAMA, WATANO WAJERUHIWA
- Runtime
- 2:57
- Date posted
- 19 days ago
- Description
- Watu sita wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa baada ya basi la abiria mali ya Kampuni ya OG Classic lililokuwa likitokea Kahama kwenda Geita kugonga lori kwa nyuma na kupinduka katika eneo la Wendele, Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.
Ajali hiyo imetokea leo Jumamosi, Juni 20, 2026 majira ya saa 12 asubuhi, ikihusisha basi hilo na lori lililokuwa likielekea Masumbwe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea ajali hiyo na kusema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo ni mwendokasi wa dereva wa basi ambaye alijaribu kulipita lori bila kuchukua tahadhari.
“Dereva wa basi alipofika eneo la Wendele alilikuta lori ambalo nalo lilikuwa likielekea Masumbwe. Alijaribu kulipita bila kuchukua tahadhari huku akiwa katika mwendokasi, ndipo alipogonga ngema na kurudi kuligonga tela la lori kisha kupinduka,” amesema Kamanda Magomi.
Amesema waliofariki katika ajali hiyo ni wanaume wanne na wanawake wa...
- Title
- SIMANZI! RPC TABORA AFARIKI DUNIA AKIPATIWA MATIBABU MUHIMBILI
- Runtime
- 1:01
- Date posted
- 19 days ago
- Description
- Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Richard Abwao amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
- Title
- WANANCHI MSIHOFU KUTUMIA NISHATI YA UMEME KATIKA VYOMBO VYA USAFIRI -TWANGE
- Runtime
- 1:47
- Date posted
- 20 days ago
- Description
- Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Lazaro Twange, amewaondoa hofu wananchi kuhusu matumizi ya nishati ya umeme katika vyombo vya usafiri, akisema kuwa Tanesco imejipanga kujenga vituo vya kuchajia vyombo hivyo nchi nzima.
Mkurugenzi huyo amesema hayo Juni 19, 2026, alipotembelea banda la Tanesco katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali, mkoani Dodoma.
Amesema shirika linatambua kuwa mahitaji ya umeme yanaendelea kuongezeka kutokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi, hivyo jitihada zinaendelea kufanyika kuhakikisha umeme unawafikia wananchi kwa ubora na uhakika kwa matumizi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.
“Tanesco inafanya kazi kubwa ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia. Aidha, sasa tunashuhudia matumizi ya umeme katika vyombo vya usafiri. Sisi kama wazalishaji wa umeme tunaonesha njia kwa kuwa tuna vyombo vingi vya usafiri vinavyotumia umeme. Tumejipanga kuj...
- Title
- KAKAMA KUWAKUTANISHA WANANCHI MATAIFA NANE MAADHIMISHO YA KISWAHILI DUNIANI
- Runtime
- 20:00
- Date posted
- 20 days ago
- Description
- Zanzibar. Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (Kakama) imetangaza maadhimisho ya Siku Kiswahili kuwakutanisha wananchi kutoka mataifa manane ya Afrika Mashariki mjini Bujumbura, Burundi.
Akizungumza leo Juni 19,2026 na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili (Kakama), Dk Caroline Asiimwe amesema maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia Julai 5-7, 2026.
Amesema maadhimisho ya Kiswahili yatatanguliwa na Kongamano la Tatu ka Kakama na kufuatiwa na Siku ya Kiswahili Duniani Julai 7.
- Title
- #live BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU, KIKAO CHA HAMSINI NA TATU JUNI 19, 2026
- Runtime
- 3:45:58
- Date posted
- 21 days ago
- Description
- #live BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU, KIKAO CHA HAMSINI NA TATU JUNI 19, 2026
- Title
- SERIKALI YAFUNGUA DIRISHA LA NNE TUZO ZA UMAHIRI WA TAFITI 2026/27
- Runtime
- 5:12
- Date posted
- 21 days ago
- Description
- Katika juhudi za kukuza na kuendeleza sayansi na teknolojia nchini, Serikali imetenga Shilingi bilioni 1.5 katika mwaka wa fedha 2025/26 kwa ajili ya Tuzo ya Umahiri kwa Tafiti na Wahadhiri kutoka taasisi za elimu ya juu za serikali na zisizo za serikali.
Tuzo hizo zitatolewa kwa watafiti ambao matokeo ya tafiti zao yatachapishwa katika majarida ya kitaaluma yenye hadhi ya juu duniani.
Hayo yameelezwa leo jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, wakati akitangaza ufunguzi wa dirisha la nne la maombi ya tuzo hizo.
Profesa Mkenda amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa tuzo hizo mwaka 2023, jumla ya machapisho 336 yalikidhi vigezo na kuingia katika ushindani. Kati ya hayo, machapisho 86 yalitunukiwa tuzo, huku jumla ya Watanzania 200 wakinufaika na tuzo hizo tangu zilipoanzishwa.
- Title
- MWALIMU ALIYETELEKEZA MKE, WATOTO MATATANI
- Runtime
- 2:24
- Date posted
- 22 days ago
- Description
- Shinyanga. Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro ameendelea kutumia mikutano ya hadhara kusikiliza na kutatua kero za wananchi, huku akitoa onyo kwa wanaume wanaokwepa majukumu ya kulea na kutunza watoto wao. Akiwa katika Tarafa ya Itwangi, amesisitiza kuwa malezi na matunzo ya watoto ni wajibu usioweza kukwepwa kwa mzazi yeyote aliyeshiriki kuwaleta duniani.
Hayo ameyazungumza leo Juni 18, 2026 katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Tarafa ya Itwangi, baada ya mkazi wa Kijiji cha Dandu C, Rukia Sosoma kudai kuwa mumewe, Seleman Ramadhan, ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Zobogo, hatoi matumizi wala kuwahudumia watoto wao na pia amekuwa akimfukuza nyumbani.
“Mume wangu hatoi matumizi na hataki kuhudumia watoto wetu akiwamo mwenye miaka tisa, mitano na wa mwisho mitatu, na pia ananifukuza nyumbani” amesema Rukia.
Imeandaliwa na Hellen Mdinda, Shinyanga.
- Title
- MSIGWA AFUNGUKA ALIVYOWEKEZA NJE YA SIASA, AITAJA YANGA
- Runtime
- 2:57
- Date posted
- 22 days ago
- Description
- Mahojiano maalumu na Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa.
Hii ni sehemu ya 4.
- Title
- #live BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU, KIKAO CHA HAMSINI NA MBILI JUNI 18, 2026
- Runtime
- 3:52:05
- Date posted
- 22 days ago
- Description
- #live BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU, KIKAO CHA HAMSINI NA MBILI JUNI 18, 2026
- Title
- MKENDA ASISITIZA USAWA WA ELIMU KWA WOTE
- Runtime
- 3:07
- Date posted
- 22 days ago
- Description
- Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda amesema elimu ni miongoni mwa vipaumbele vikuu vya taifa, huku serikali ikiendelea kusisitiza usawa wa elimu kwa watoto wote bila ubaguzi wa kijinsia.
Akizungumza kuhusu mazingira ya kujifunzia, Mkenda amesema hata mabinti waliopata ujauzito wanaruhusiwa na wanapaswa kurejea shuleni ili kuendelea na masomo yao.
Ameeleza kuwa ili kuhakikisha watoto wote wanahudhuria shule, ni muhimu kuwepo mazingira bora ikiwemo usafi, vyoo vya viwango vinavyokubalika, maeneo ya faragha na vyumba maalumu vya kujisitiri kwa wanafunzi wa kike.
- Title
- WHY BANKING IS STILL A TRUST BUSINESS.
- Runtime
- 47:51
- Date posted
- 22 days ago
- Description
- Three years into leading Absa Bank Tanzania, Managing Director and CEO Obedi Laiser says the bank’s next phase of growth will depend less on scale and more on trust, innovation and disciplined execution.
In this interview, he talks about navigating a highly concentrated banking market, reducing reliance on traditional lending and building a more diversified digital business. He also discusses competition from fintechs, the barriers facing women entrepreneurs, the role of local leadership and how success should ultimately be measured beyond financial performance.
- Title
- #Live: BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU, KIKAO CHA HAMSINI NA MOJA JUNI 17, 2026
- Runtime
- 3:55:21
- Date posted
- 22 days ago
- Description
- #Live: BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU, KIKAO CHA HAMSINI NA MOJA JUNI 18, 2026
- Title
- DC SIHA AFUNGUKA KUHUSU VURUGU ZILIZOTOKEA KWENYE MAZISHI, JENEZA KUWEKWA KWENYE GARI LAKE
- Runtime
- 3:44
- Date posted
- 22 days ago
- Description
- Wakati mwili wa kijana Emmanuel Mwandry(20) ukizikwa chini ya ulinzi wa Jeshi la polisi saa 2:30 usiku jana baada ya kuibuka vurugu katika mazishi yake, Mkuu wa wilaya ya Siha, Mkoani Kilimanjaro, Dk Christopher Timbuka amefunguka na kusimulia kilichotokea.
Vurugu hizo zilitokana na madai ya kukamatwa kwa madereva wenzao mjini Moshi ambao walikuwa kwenye msafara wa kwenda kuchukua mwili hospitali ya Rufaa ya kanda ya Kaskazini, KCMC.
Kutokana na vurugu hizo madereva hao wa bodaboda walizuia shughuli za mazishi kuendelea nyumbani kwa wazazi wa marehemu hadi usiku ndipo mkuu wa wilaya hiyo alipolazimika kufika msibani hapo na kutuliza vurugu hizo bila mafanikio.
- Title
- KIKUNDI CHA KILUA KUKIWASHA UZINDUZI WA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA ZANZIBAR
- Runtime
- 1:34
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- Burudani ya aina ya kipekee inatarajiwa kuwa sehemu ya mvuto mkubwa katika uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, Zanzibar, baada ya kikundi cha Ngoma ya Kilua kuthibitisha ushiriki wake katika tukio hilo.
Wanakikundi wa ngoma hiyo wametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi, wakisisitiza kuwa mbali na burudani, wananchi pia watapata fursa ya kunufaika na huduma za msaada wa kisheria zitakazotolewa bure.
Uzinduzi unatarajiwa kufanyika Juni 20, 2026 katika Viwanja vya Dole Kizimbani, Zanzibar. Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Ngoma ya Kilua ni moja ya ngoma za kitamaduni zenye asili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo baadaye ilisambaa na kupata umaarufu mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki, ikiwemo Visiwa vya Zanzibar.
- Title
- #Live: BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU, KIKAO CHA HAMSINI TAREHE JUNI 16, 2026
- Runtime
- 3:48:37
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- #Live: BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU, KIKAO CHA HAMSINI TAREHE JUNI 16, 2026
- Title
- #Live: BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU, KIKAO CHA HAMSINI TAREHE JUNI 16, 2026
- Runtime
- 35:03
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- #Live: BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU, KIKAO CHA HAMSINI TAREHE JUNI 16, 2026
- Title
- Bodaboda wagoma kuzika,Waweka Jeneza Juu ya Gari la DC
- Runtime
- 3:18
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- Siha. Vurugu zimesitisha mazishi ya kijana Emmanuel Mwandry katika kijiji cha Ngirinyi, Kata ya Nasai wilayani Siha mkoani Kilimanjaro baada ya kundi la vijana bodaboda kugoma kuendelea na shughuli za mazishi wakishinikiza kuachiwa kwa wenzao wanaodaiwa kukamatwa na Jeshi la Polisi.
Hali ilizidi kuwa tete baada ya vijana hao kulichukua jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu na kuliweka juu ya gari la Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dk Christopher Timbuka, wakidai hawataruhusu mazishi kuendelea hadi wenzao waliokamatwa wakati wa msafara wa kuchukua mwili kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC waachiwe.
Taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa baadhi ya waendesha bodaboda walikamatwa asubuhi ya Juni 16, 2026 katika eneo la KCMC wakati wa vurugu zilizotokea wakati wa taratibu za kuchukua mwili wa marehemu aliyefariki Juni 12 mwaka huu katika mazingira yanayodaiwa kuhusisha gari la polisi lililokuwa likimkimbiza.
Baada ya mwili kufikishwa nyumbani ...
- Title
- #Live: BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU, KIKAO CHA AROBAINI NA TISA TAREHE JUNI 15, 2026
- Runtime
- 47:23
- Date posted
- 24 days ago
- Description
- LIVE: BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU, KIKAO CHA AROBAINI NA TISA TAREHE JUNI 15, 2026
- Title
- Muhongo apendekeza sekta saba kukuza uchumi wa Tanzania
- Runtime
- 8:33
- Date posted
- 24 days ago
- Description
- Mbunge wa Musoma Vijijini, Sospeter Muhongo, ametaja maeneo saba muhimu kwa ajili ya kukuza uchumi, huku akisisitiza Bunge kuipitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2026/27 kwa kuwa inalenga kuharakisha ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini.
Amesema Tanzania inapaswa kuwekeza zaidi katika uchumi unaotegemea maarifa, kilimo na viwanda vyake, gesi asilia, madini ya kimkakati, utalii, uvuvi, ufugaji, pamoja na kuimarisha usafirishaji wa nguvu kazi kwenda nje ya nchi.
Aidha, amependekeza sekta za michezo, muziki na sanaa zipewe kipaumbele kwa kuwa zina uwezo wa kuongeza mchango katika Pato la Taifa.
Muhongo amesisitiza umuhimu wa kuwa na umeme wa uhakika na wa gharama nafuu, kuongeza akiba ya dhahabu kupitia Benki Kuu, pamoja na kuanzisha mfuko maalumu wa kuhifadhi mapato ya madini kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Muhongo, akirejea ripoti ya African Development Bank (AfDB), amesema uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua kwa asilimia 6.1 mwaka 2027 huku mfum...
- Title
- WATOTO WATATU WALIOPOTEA LINDI WAKUTWA PORINI WAMENYONGWA, WAKATWA VIUNGO, MAMA MZAZI AFUNGUKA ...!
- Runtime
- 5:55
- Date posted
- 25 days ago
- Description
- Watoto watatu wa familia moja, wakazi wa Kijiji cha Kilimahewa wa Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi waliopotea Juni 8, 2026 wakiwa njiani kwenda madrasa wamekutwa wamefariki dunia kwa kunyongwa.
Watoto hao ni Kulwa Mohamed (7) na Doto Mohamed (7), wanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Mitopitopi pamoja na Rehema Mohamed (6), mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Mpanyu.
Miili ya watoto hao ilipatikana kwa nyakati tofauti ambapo miwili ilipatikana Juni 13, 2026 na mmoja ulipatikana asubuhi ya jana Jumapili Juni 14, 2026 yote katika Pori la Kijiji cha Kilimawe.
Jana Jumapili, Juni 14, 2026, miili ya watoto hao ilizikwa ambapo viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi (RC), Zainab Telack walishiriki.
Akielezea tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori alisema watoto hao walitoka nyumbani kwao Juni 8 kwenda madrasa ambako taarifa walizonazo hawakufika na kupotelea njiani ambapo walianza msako ku...
- Title
- MFUPA ULIOMSHINDA BABA CCM, MWANAYE AUWEZA AKIWA UPINZANI
- Runtime
- 10:57
- Date posted
- 25 days ago
- Description
- Mahojiano Maalumu na mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kiza Mayeye kuanzia.
- Title
- INSIDE TANZANIA-AUSTRALIA BILATERAL TIES
- Runtime
- 26:31
- Date posted
- 25 days ago
- Description
- Outgoing Australian High Commissioner Jenny Da Rin opens up on successes and lessons from her time in Tanzania and East Africa.
- Title
- MTENDAJI ANUSURIKA KUWEKWA NDANI KUTOHUDHURIA KIKAO
- Runtime
- 4:36
- Date posted
- 25 days ago
- Description
- Shinyanga. Mtendaji wa Kata ya Salawe, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, George Kuchibanda, amenusurika kuwekwa ndani baada ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi yanayomhusu mtendaji huyo, huku yeye mwenyewe akiwa hayupo katika hadhara hiyo kujibu malalamiko hayo.
Akizungumza leo Juni 14, 2026, katika ziara yake, Mtatiro ameagiza kuwa mtendaji huyo atafutwe haraka na aende kueleza kwa nini hajahudhuria mkutano huo wakati viongozi na watumishi wa Serikali ya wilaya wanatakiwa kuwepo. Amesema kama hatakuwa na majibu ya kuridhisha, awekwe ndani na wakutane naye kesho ili iwe funzo kwa wengine.
Malalamiko hayo yametolewa na mkazi wa Kijiji cha Songambele, Kata ya Salawe, Nkonya Mathias, akilalamika kuwa vijana wa kijiji hicho walifukuzwa na watu walioongozwa na mtendaji huyo katika stendi na kukatazwa kufanya biashara zao, jambo lililosababisha vurugu.
Mwananchi mwingine kutoka kata hiyo, Kanisio Maga...
- Title
- MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI MKOMBOZI MIGOGORO YA MIPAKA YA VIJIJI MSALALA
- Runtime
- 3:11
- Date posted
- 25 days ago
- Description
- Zaidi ya wananchi 800 kutoka vijiji tisa vya Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga, wanatarajiwa kunufaika na mpango wa matumizi ya ardhi, ikiwa ni jitihada za serikali kuhakikisha ardhi inatumika kuimarisha maendeleo ya jamii za vijijini.
Mwenyekiti wa kijiji cha Nata, kata ya Mwanase, Msalala, Charles Bulugu Juni 13, 2026, ameomba kuharakishwa mchakato wa upimaji wa maeneo ya kijiji ili kutambua mipaka ya kijiji hicho na kutatua mgogoro wa mpaka wa kijiji uliodumu kwa miaka 24.
Amesema “Tunashukuru huu mpango kutufikia, uharakishwe ili tuijue mipaka ya kijiji hiki na Mwakuhenga. Kuna eneo la kilimo hapa lakini sisi hatulimi na wale hawalimi kwa sababu kila mmoja anadhani ni kwake tangu mwaka 2002.”
Afisa mipango miji kutoka Tume ya Taifa ya Mpango wa matumizi ya ardhi Abdallah Magombana, amesema ukamilishaji wa shughuli hiyo, utakuwa suluhisho la migogoro ya muda mrefu, na wananchi wataendelea na shughuli zao za kiuchumi.
Ames...
- Title
- Ulikuwa unafahamu hili?
- Runtime
- 1:58
- Date posted
- 25 days ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- NDOINYO ATAJA KITAKACHOMALIZA CHANGAMOTO NGORONGORO
- Runtime
- 17:52
- Date posted
- 25 days ago
- Description
- Dodoma. Mbunge wa Ngorongoro, Yannick Ndoinyo amesema ushirikishwaji wa wananchi na kusikilizwa kwa maoni yao, ndiyo njia itakayomaliza changamoto zinazoikabili Ngorongoro, badala ya kutegemea uhamishaji wa watu pekee.
Ndoinyo amesema wananchi wengi wa wilaya hiyo hawataki kuhama kutoka maeneo yao ya asili, licha ya kuunga mkono juhudi za uhifadhi zinazoendelea katika eneo hilo. Amesisitiza kuwa kupata suluhu ya kudumu kuhusu hatima ya Ngorongoro kunahitaji mazungumzo ya wazi na kuwashirikisha wananchi katika maamuzi yanayohusu maisha yao na mustakabali wa eneo hilo.
Kauli hiyo imekuja wakati Ngorongoro ikiendelea kuwa kitovu cha mjadala wa kitaifa kuhusu namna bora ya kusawazisha masilahi ya uhifadhi na ustawi wa jamii zinazoishi ndani ya eneo la hifadhi.
Hoja za mbunge huyo zinafanana na yale yaliyobainishwa na tume iliyoundwa kuchunguza mchakato wa uhamishaji wa wananchi katika eneo hilo, ambayo ilieleza kuwa baadhi ya wananchi hawakuwa tayari ...
- Title
- HAYA NDIYO MAZISHI MZEE ONYANGO MAKABURI YA KONDO DAR
- Runtime
- 3:28
- Date posted
- 26 days ago
- Description
- Hivi ndivyo mwili wa msanii mkongwe Issa Mohamed maarufu Mzee Onyango ulivyozikwa katika makamburi ya Kondo yaliyopo Ununio, Dar es Salaam leo Juni 13, 2026.
Mzee Onyango alifariki dunia usiku wa kuamkia Alhamisi, Juni 11, 2026, katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mtoto wake, Joseph Issa, marehemu alifariki majira ya saa saba usiku baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa shinikizo la damu.
- Title
- TANZANIA YAFUNGUA RASMI SOKO LA NDIZI AFRIKA KUSINI
- Runtime
- 7:41
- Date posted
- 26 days ago
- Description
- Tanzania imefungua rasmi soko la ndizi mbichi nchini Afrika Kusini baada ya kukamilika kwa majadiliano ya kitaalamu kuhusu matakwa ya afya ya mimea kati ya mamlaka husika za nchi hizo mbili.
Hatua hiyo imefikiwa kupitia mazungumzo kati ya Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) na Mamlaka ya Afya ya Mimea ya Afrika Kusini (NAPOZA), yaliyolenga kuridhiana kuhusu masharti ya afya ya mimea yanayoruhusu ndizi kutoka Tanzania kuingia katika soko la nchi hiyo.
Aidha, mauzo ya nje ya mazao ya kilimo ya Tanzania kwa sasa yanakadiriwa kufikia thamani ya takribani dola za Marekani bilioni 3.54 (sawa na zaidi ya shilingi trilioni 9.3 za Tanzania) kwa mwaka.
Kwa upande wa ndizi pekee, mauzo yake ya nje yanakadiriwa kuwa na thamani ya takribani dola za Marekani milioni 3.67 (zaidi ya shilingi bilioni 9.6 za Tanzania) kwa mwaka, yakipelekwa katika masoko mbalimbali yakiwemo Zambia, Malawi, Uganda na nchi za Umoja wa Ulaya (EU).
Ufun...
- Title
- RAIS MWINYI ALIVYOAGA MWILI WA MZEE ONYANGO
- Runtime
- 1:18
- Date posted
- 26 days ago
- Description
- Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi ni miongoni mwa waombolezaji waliojitokeza kuuaga mwili wa msanii mkongwe Issa Mohamed maarufu Mzee Onyango, Kawe jijini Dar es Salaam.
Mzee Onyango alifariki dunia usiku wa kuamkia Alhamisi, Juni 11, 2026, katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mtoto wake, Joseph Issa, marehemu alifariki majira ya saa saba usiku baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa shinikizo la damu.
Marehemu Mzee Onyango anatarajiwa kuzikwa leo, Jumamosi, Juni 13, 2026, katika Makaburi ya Kondo yaliyopo Ununio, Dar es Salaam.
- Title
- MSAFARA ULIOBEBA MWILI WA MZEE ONYANGO UKIELEKEA MAKABURINI
- Runtime
- 4:10
- Date posted
- 26 days ago
- Description
- Msanii Issa Mohamed ‘Mzee Onyango’ alifariki dunia usiku wa kuamkia Alhamisi, Juni 11, 2026, katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mtoto wake, Joseph Issa, baba yake alifariki majira ya saa saba usiku baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa shinikizo la damu.
Marehemu Mzee Onyango anatarajiwa kuzikwa leo, Jumamosi, Juni 13, 2026, katika Makaburi ya Kondo yaliyopo Ununio, Dar es Salaam.
- Title
- MWANA FA AFICHUA YA MAREHEMU MZEE ONYANGO ENZI ZA UHAI WAKE
- Runtime
- 4:45
- Date posted
- 26 days ago
- Description
- Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma 'Mwana FA', amesema marehemu Issa Mohamed ‘Mzee Onyango’ alikuwa nyota mkubwa wa sanaa ya maigizo na ucheshi nchini, ambaye mchango wake ulihamasisha na kuvutia wasanii wengi kujikita katika tasnia ya sanaa kutokana na umahiri wake mkubwa wa kuigiza.
Msanii huyo mkongwe alifariki dunia usiku wa kuamkia Alhamisi, Juni 11, 2026, katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mtoto wake, Joseph Issa, baba yake alifariki majira ya saa saba usiku baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa shinikizo la damu.
Marehemu Mzee Onyango anatarajiwa kuzikwa leo, Jumamosi, Juni 13, 2026, katika Makaburi ya Kondo yaliyopo Ununio, Dar es Salaam.
- Title
- MSIGWA: NILIVYOZIFANYA GWANDA ZA CHADEMA, NGUO ZA CCM ITABAKI ...
- Runtime
- 7:44
- Date posted
- 27 days ago
- Description
- Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa alipoulizwa swali kuhusu alikozipeleka gwanda za Chadema mara baada ya kujiunga na CCM, na nguo za CCM baada ya kukikacha chama hicho na kurejea tena Chadema amesema hilo ni siri ya kambi.
Mchungaji Msigwa ambaye alikuwa mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chadema kwa miaka 10 (2010-2020), alijiunga na CCM Juni 30, 2024 kabla ya kutangaza kurejea Chadema Mei 23, 2026 huku akitoa sababu kuu kwamba mauaji ya Oktoba 29, 2025 yalisukuma dhamira yake.
Mwananchi lilifanya mahojiano maalumu na Msigwa Jumanne Juni 2, 2026, jijini Dar es Salaam kuhusu uamuzi wake wa kuondoka CCM alikokaa takribani miaka miwili na kurejea Chadema ambako aliwahi kuwa mbunge na mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa.
Akizungumzia uamuzi wa kurejea Chadema, Mchungaji Msigwa amesema alitumia miezi sita kutafakari kuhusu uamuzi wake wa kuondoka CCM kutokana na mauaji ya wananchi yaliyofanyika wakati na baada ya uchaguz...
- Title
- #Live: RAIS SAMIA AKISHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA BENKI KUU YA TANZANIA, JNICC DAR ES SALAAM
- Runtime
- 2:10:16
- Date posted
- 27 days ago
- Description
- RAIS SAMIA AKISHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA BENKI KUU YA TANZANIA, JNICC DAR ES SALAAM
- Title
- AKIBA YA DHAHABU BoT YAFIKIA TANI 27.5 ZENYE THAMANI YA SH10 TRILIONI
- Runtime
- 2:03
- Date posted
- 28 days ago
- Description
- Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema hadi kufikia Juni 10, 2026 ina akiba ya dhahabu ya tani 27.5 yenye thamani inayokadiriwa kufikia takribani Sh10 trilioni.
Hayo yamesemwa leo Ijumaa, Juni 12, 2026 na Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba, wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Benki Kuu ya Tanzania yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ndiye mgeni rasmi.
Tutuba amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Benki Kuu kuimarisha akiba ya taifa na kuongeza uthabiti wa uchumi wa nchi kupitia uwekezaji katika madini ya dhahabu kama mali salama ya kifedha.
“Mpaka kufikia Juni 10, 2026, Benki Kuu ina dhahabu tani 27.5 zenye thamani ya takribani Sh trilioni 10,” amesema Tutuba.
Aidha, BoT imekuwa ikiweka wazi mkakati wake wa kuongeza akiba ya dhahabu kwa kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wa ndani kupitia utaratibu rasmi wa kibenki. Hatua hiyo imekuwa ...
- Title
- RAIS SAMIA AZINDUA KITABU MAADHIMISHO YA BoT MIAKA 60, IPO ALBAMU YA NOTI
- Runtime
- 4:07
- Date posted
- 28 days ago
- Description
- Rais Samia Suluhu Hassan amezindua kitabu maalumu cha maadhimisho ya miaka 60 ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kinachojumuisha albamu ya matoleo mbalimbali ya noti zilizotumika nchini kuanzia mwaka 1966 hadi 2026.
Uzinduzi huo umefanyika leo, Juni 12, 2026, katika kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), yanayofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), jijini Dar es Salaam.
- Title
- BoT YAADHIMISHA MIAKA 60 IKIANZISHA KITENGO CHA AKILI UNDE
- Runtime
- 3:26
- Date posted
- 28 days ago
- Description
- Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeanzisha kitengo cha Akili Unde (AI) na ikisaini mikataba na vyuo vikuu sita nchini kwa lengo la kuimarisha uwezo wa kuchakata takwimu na kufanya maamuzi kwa kutumia taarifa zinazozalishwa na mifumo ya akili unde.
Hayo yameelezwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba, ambaye amesema hatua hiyo imechochewa na ukuaji wa teknolojia za kifedha pamoja na ubunifu mpya unaoendelea kujitokeza duniani.
Ameongeza kuwa BoT imeendelea kuimarisha mifumo ya kudhibiti vihatarishi vinavyojitokeza katika huduma za malipo ya kidijitali, ili kuhakikisha teknolojia hizo zinaongeza ufanisi, kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha na kuimarisha uthabiti wa fedha bila kuleta uhararishaji wa fedha nchini.
Tutuba ameyasema hayo leo Ijumaa Juni 12, 2026 wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yanayofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre jijini Dar ...
- Title
- Wananchi Vijibweni waibua kero za barabara, shule na migogoro ya ardhi mbele ya Chalamila
- Runtime
- 8:06
- Date posted
- 28 days ago
- Description
- Dar es Salaam.
Wananchi wa Mtaa wa Vijibweni, Wilaya ya Kigamboni, wameiomba Serikali kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili, zikiwemo ubovu wa barabara, uhaba wa madarasa na madawati shuleni pamoja na migogoro ya ardhi, wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ya kukagua miradi ya maendeleo katika eneo hilo.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika wakati wa ziara hiyo, wananchi walieleza kutoridhishwa na hali ya Barabara ya Soweto ambayo imeendelea kuwa kero kwa muda mrefu. Walidai kuwa matengenezo ya barabara hiyo yamekuwa yakifanyika kwa muda mfupi kila viongozi wanapotembelea eneo hilo, lakini husimama mara baada ya ziara hizo kukamilika.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Vijibweni, Mohamed Zigo, alisema juhudi zinazofanywa na wakandarasi zimekuwa za muda mfupi na kushindwa kutoa suluhisho la kudumu kwa changamoto ya miundombinu ya barabara. Alisema hali hiyo imeendelea kuathiri shughuli za kiuchumi na u...
- Title
- #Live: BAJETI KUU YA SERIKALI IKISOMWA BUNGENI DODOMA
- Runtime
- 1:52:05
- Date posted
- 28 days ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- #live HAFLA YA UTIAJI SAINI NA UZINDUZI WA MIRADI YA NISHATI SAFI
- Runtime
- 22:50
- Date posted
- 28 days ago
- Description
- #live HAFLA YA UTIAJI SAINI NA UZINDUZI WA
MIRADI YA NISHATI SAFI
- Title
- WANANCHI USANDA WALIA UHABA WA MAJI, RUWASA YAJIBU
- Runtime
- 3:20
- Date posted
- 28 days ago
- Description
- Shinyanga. Katika kliniki ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro inayohusiana na kusikiliza na kutatua kero za wananchi iliyoanza katika kata na Tarafa ya Samuye Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga, wananchi walia na changamoto ya maji huku wakiomba kuchimbiwa kisima kitakacho wasaidia kwa muda ambao watakuwa wakisubiri ujio wa maji ya ziwa Viktoria.
Akizungumza leo Juni 11, 2026 katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi, mkazi wa Kata ya Usanda George William Shija ameeleza kuwa kero hiyo imekuwa kwa muda mrefu na kwa muda mwingine wakazi wa mbali na mto huo wamekuwa wakiuziwa maji kutoka mto huohuo,
“Changamoto yangu ni maji ya mto tunayotumia si salama, nakero ya maji katika eneo hili imekuwepo kwa muda mrefu hatuna maji safi na salama, pia maji haya haya tunakunywa na kuchangia na mifugo, tunaomba angalau tuchimbiwe kisima cha maji kwa muda ambao tunasubiria kuunganishiwa maji ya ziwa Viktora” amesema Shija.
- Title
- #Live: BAJETI KUU YA SERIKALI IKISOMWA BUNGENI DODOMA
- Runtime
- 0:00
- Date posted
- 28 days ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- #live HAFLA YA UTIAJI SAINI NA UZINDUZI WA MIRADI YA NISHATI SAFI
- Runtime
- 2:26:03
- Date posted
- 29 days ago
- Description
- #live HAFLA YA UTIAJI SAINI NA UZINDUZI WA
MIRADI YA NISHATI SAFI

