Mwananchi Digital
KINDAMBA NAMLIA AFUNGUKA KINACHOIKWAMISHA STARS
- Title
- KINDAMBA NAMLIA AFUNGUKA KINACHOIKWAMISHA STARS
- Runtime
- 6:44
- Date posted
- 2 hours ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- MAJONGORO NYERERE AIANGUKIA SERIKALI BAADA YA TAMASHA LA CHEKA TU
- Runtime
- 8:22
- Date posted
- 5 hours ago
- Description
- Msanii Majongoro Nyerere anayejitambulisha kwa muonekano wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, amesema ameamua kutumia sanaa hiyo kuendeleza ujumbe wa uzalendo na kumuenzi Nyerere, akisema popote penye watu ndipo ujumbe unapaswa kufikishwa.
Amesema anatamani kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwa kutumia taswira ya Nyerere, huku akiahidi kuendeleza sanaa hiyo kwa mUOnekano, sauti na mienendo inayofanana na Baba wa Taifa.
- Title
- JJ AVUNJA UKIMYA ‘LAST DANCE’ YA CHEKA TU
- Runtime
- 9:06
- Date posted
- 5 hours ago
- Description
- Msanii wa vichekesho JJ Ephraim amezungumzia kauli ya kutajwa kwa onyesho la Cheka Tu kuwa lililofanyika kama ‘Last Dance’, akisema huenda ilikuwa mwisho wa mfumo uliokuwa ukitumika kwa muda mrefu, badala ya kuwa mwisho wa maonyesho hayo.
JJ Ephraim amesema anaamini Cheka Tu inaweza kurejea kwa mfumo mwingine, huku akieleza kuwa endapo maonyesho hayo yangefikia mwisho kabisa, angeumia kwa kuwa yamekuwa sehemu muhimu ya tasnia ya vichekesho.
- Title
- NDARO: CHEKA TU IKIFA ITANIUMA SANA
- Runtime
- 2:40
- Date posted
- 7 hours ago
- Description
- Msanii wa vichekesho Ndaro, ambaye ni mmoja wa wasanii wanaounda kundi la Cheka Tu, amesema tamasha la kundi hilo lililofanyika jana limekuwa zuri kutokana na mashabiki kupata nafasi ya kukutana na wasanii hao baada ya muda mrefu, furaha yao ilikuwa kubwa zaidi.
Ndaro amesema licha ya mashabiki kufurahia kurejea kwao jukwaani, wasanii nao wamefurahi zaidi kwa sababu wamepata nafasi ya kukutana na mashabiki waliokuwa wakiwakosa kwa muda.
Amesema endapo kundi la Cheka Tu litafikia mwisho, jambo hilo litamuumiza kwa kuwa kundi hilo limekuwa na mchango mkubwa katika kuwapa vijana wenye vipaji vya ucheshi jukwaa la kuonyesha uwezo wao na kujenga majina katika tasnia hiyo.
“Shoo ya leo ilikuwa nzuri, mashabiki wamefurahi kwa sababu muda mrefu hatujakutana nao, lakini sisi tumefurahi zaidi. Kama kweli Cheka Tu itakufa, mimi itauma sana kwa sababu hili ni moja ya majukwaa yanayowapa vijana nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kuwafikisha juu,” amesema N...
- Title
- HAFLA YA UTIAJI SAINI ΜΚΑΤΑΒA WA UFADHILI WA UUNGANISHAJI UMEME KWA WANANCHI KATI YA TANESCO NA CRDB
- Runtime
- 2:55:00
- Date posted
- 9 hours ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- AGA KHAN YAWEKEZA SH1.3 BILIONI, YAONGEZA UWEZO TIBA YA KINYWA, KUREJESHA UTENDAJI WA MENO
- Runtime
- 6:24
- Date posted
- 15 hours ago
- Description
- Hospitali ya Aga Khan imezindua kliniki yake iliyoboreshwa ya afya ya kinywa na meno, hatua inayolenga kuongeza uwezo wa wagonjwa kupata matibabu ya kisasa nchini. Kliniki hiyo sasa ina uwezo wa kutoa huduma mbalimbali, ikiwamo vipandikizi vya meno, upangaji wa meno, urejeshaji wa meno, uchunguzi na huduma za kinga.
Kliniki hiyo iliyozinduliwa leo Ijumaa, Oktoba 2, 2026 baada ya uwekezaji wa Sh1.3 bilioni, ina vyumba sita vya matibabu vilivyowekwa vifaa vya kisasa kwa ajili ya huduma kwa watoto na watu wazima.
Kwa wagonjwa waliopoteza au kuharibika meno, uwekezaji huo unaongeza upatikanaji wa huduma za kurejesha utendaji na mwonekano wa meno. Pia, wenye matatizo ya mpangilio wa meno wanaweza kupata huduma za orthodontics, huku uchunguzi na huduma za kinga zikisaidia kugundua matatizo ya afya ya kinywa mapema.
Mkurugenzi wa Tiba wa Hospitali ya Aga Khan, Dk Muzdalifat Abeid, amesema uwekezaji huo unalenga kuongeza upatikanaji wa huduma za meno ze...
- Title
- MC GARA B: NILIANZA KAZI YA MC KWA KUVAMIA HARUSI
- Runtime
- 31:09
- Date posted
- 17 hours ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- SERIKALI KUFUNGUA DIRISHA LA PILI BIMA YA AFYA KWA WOTE
- Runtime
- 2:10
- Date posted
- 18 hours ago
- Description
- Serikali imetangaza kufungua dirisha la pili la utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, hatua itakayotoa fursa kwa Watanzania wengi zaidi kujiunga na mfumo huo.
Akizungumza leo Oktoba 2, 2026 wakati akizindua kliniki ya meno ya Hospitali ya Aga Khan, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya anayeshughulikia Dawa na Vifaa Tiba, Emmanuel Tayari, amesema dirisha hilo litamalizia usajili wa kaya zisizo na uwezo na wakati huohuo kufungua fursa kwa makundi yote maalum, huku utaratibu kamili ukitarajiwa kutangazwa hivi karibuni.
“Katika awamu ya pili tutamalizia kusajili zile kaya za maskini, lakini tutafungua kwa makundi yote maalum. Kwa maana hiyo, Watanzania wote watakaribishwa au kuhimizwa kujiunga,” amesema.
Serikali imeanza utekelezaji tangu Januari 26, 2026, ambapo kaya 276,004 ziliainishwa kunufaika na bima inayogharamiwa na Serikali. Hadi Juni mwaka huu, wanufaika 997,015 kati ya waliolengwa 1,206,319 walikuwa wamesajiliwa.
Tayari ames...
- Title
- TANROADS YABORESHA MABANGO YA MAELEKEZO DAR, MADEREVA WAPONGEZA
- Runtime
- 5:32
- Date posted
- 19 hours ago
- Description
- Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam umeanza kuboresha na kufunga mabango mapya ya maelekezo katika maeneo mbalimbali ya jiji, hatua ambayo imepongezwa na madereva wakisema itarahisisha utambuzi wa maeneo na mwelekeo kwa watumiaji wa barabara.
Mabango hayo mapya yenye ukubwa na urefu zaidi yameanza kuonekana katika baadhi ya barabara na makutano, yakionyesha majina ya maeneo pamoja na mwelekeo wa kwenda katika maeneo mbalimbali ya jiji.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam, Lazeck Kyamba, amesema mabango hayo yamewekwa baada ya kubaini kuwa baadhi ya yaliyokuwepo yalikuwa yamechakaa au kuharibika baada ya kugongwa, huku mengine yakiwa madogo kiasi cha kutokuonekana kwa urahisi.
“Mabango haya yana herufi kubwa sana na yanaonyesha direction ya wapi unakwenda. Mengi yalikuwa yamegongwa lakini mengine yalikuwa machakavu. Sasa tunayarudisha, tunaanza kuyafunga na kuyaboresha zaidi,” amesema Kyamba.
Amesema u...
- Title
- WACHIMBAJI WADOGO WAONYWA KUCHIMBA KWA KUBAHATISHA
- Runtime
- 2:28
- Date posted
- 20 hours ago
- Description
- Shinyanga. Wakati Serikali ikiweka nguvu kuinua sekta ya madini kupitia utafiti, baadhi ya wataalamu binafsi wamesema jitihada hizo zitainua sekta hiyo kiuchumi, huku Serikali ikilenga kuongeza utafiti kutoka asilimia 16 hadi asilimia 50 ifikapo 2050.
Akizungumza leo Oktoba 2, 2026 katika maonesho ya madini mkoani Geita, Mkurugenzi Mtendaji wa Abotec Mining Sercices na One4S Mining Services, Geofrey Mwaselela amesema wachimbaji wadogo wamechelewa kufanikiwa kutokana na imani za kishirikina,
“Wachimbaji wanatakiwa kuacha kuchimba kwa kubahatisha, ukimshauri hili eneo siyo sahihi adai mtaalamu wake kamwambia achimbe hapo, akitaka kubadili eneo hadi amuulize mtaalamu, lakini elimu imeendelea kutolewa na kwa sasa wanasikiliza ushauri,” amesema Mwaselela.
Naye Mhandisi wa Madini Martha Mwakajaba amesema kwa sasa jamii imeanza kuelimika huku wakishirikiana na Serikali kufanya tafiti. “Kwa sasa jamii ya wachimbaji imeanza kuelimika tofauti na zama...
- Title
- ASKARI 3 WAJERUHIWA BAADA YA GARI LA POLISI KUGONGA MTI
- Runtime
- 2:12
- Date posted
- 2 days ago
- Description
- Title
- MACHINGA MANZESE WAUZA KWA HOFU, MBEZI WAPANGWA
- Runtime
- 5:51
- Date posted
- 2 days ago
- Description
- Dar es Salaam. Wakati baadhi ya wafanyabiashara ndogo ndogo eneo la Mbezi wakihamia katika maeneo rasmi yaliyotengwa kwa ajili ya biashara, machinga wa Manzese wameeleza hofu kuhusu hatma ya biashara zao baada ya muda waliotakiwa kuondoka kwa hiari kupita,
Mwananchi Digital imetembelea masoko ya Mbezi na Manzese, Manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam, ambako Machinga walipewa muda hadi Septemba 29, 2026 kuondoka kwa hiari katika maeneo yasiyo rasmi kabla ya kuanza kuondolewa kwa lazima.
Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, Septemba 2, 2026, kuwaagiza wakuu wa mikoa kusimamia upangaji wa wafanyabiashara wadogo katika maeneo rasmi bila kutumia nguvu.
Leo Oktoba 1, 2026, Mwananchi Digital imeshuhudia baadhi ya machinga wa Mbezi wakihamia katika maeneo rasmi ya soko, huku wengine wakisema bado wanakusanya fedha kwa ajili ya kuboresha vibanda walivyotengewa.
Mwenyekiti wa Machinga Manzese, Hashim Salum, amesema hali hiyo ina...
- Title
- UMRI WA KUISHI WAPANDA UHITAJI TIBA SHUFAA WAKUA/ KONGAMANO KUBWA LA TIBA SHUFAA KUFANYIKA DAR
- Runtime
- 6:07
- Date posted
- 2 days ago
- Description
- Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam DK. MOHAMED MANG’UNA, amesema wakati Umri wa kuishi kwa Watanzania ukizidi kuongezeka hadi kufikia zaidi ya miaka 60, uhitaji wa tiba shufaa utaongezeka kutokana na matarajio ya kuwa na Idadi kubwa ya Wazee miaka ijayo.
Tiba shufaa inahusisha huduma maalum ya matibabu inayolenga kuboresha maisha ya wagonjwa wenye magonjwa sugu na ambao wameumwa kwa muda mrefu.
Wagonjwa wenye saratani, magonjwa ya moyo na figo, kiharusi, pamoja na changamoto za afya ya akili wanalengwa zaidi na huduma hii.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, DK. Mohamed Mang’una anasema kutokana na umri wa kuishi kwa Watanzania kuongezeka hadi kufikia miaka zaidi ya 60 kuna haja ya kuweka nguvu zaidi kwenye Tiba shufaa ili kusaidia Idadi kubwa ya wazee miaka ijayo.
Hayo yanajiri ikiwa ni maandalizi ya Kongamano la nne la Kisayansi la tiba shufaa Afrika Mashariki linalotarajiwa kufanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuanzia Octoba Mosi na mbili Mwa...
- Title
- SIKU YA WAZEE: UZEE HAUONDOI THAMANI YA MTU
- Runtime
- 19:17
- Date posted
- 3 days ago
- Description
- Leo, Oktoba Mosi, dunia inaadhimisha Siku ya Wazee, lakini kwa Tanzania, siku hiyo inaibua mjadala mpana kuhusu namna jamii inavyowatambua wazee, kulinda haki zao na kuhakikisha wanaendelea kushiriki kikamilifu katika maisha ya jamii.
Akizungumza na Mwananchi Septemba 29, 2026 Dk Hellen Kijo-Bisimba amesema kufikisha miaka 60 au zaidi hakumaanishi mtu amepoteza uwezo wa kufikiri, kufanya maamuzi au kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii.
Anasema mabadiliko makubwa yanayotokea mtu anapozeeka yako zaidi kwenye mwili, si kwenye utu, fikra wala thamani yake kama binadamu.
- Title
- Kayange: Kilichonikuta Sauzi kimenifunza mengi
- Runtime
- 17:21
- Date posted
- 3 days ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- MGOMO WA MADEREVA WAENDELEA KILIMANJARO, ABIRIA WAKISOTA STENDI YA MOSHI
- Runtime
- 6:23
- Date posted
- 3 days ago
- Description
- Moshi. Abiria wanaosafiri kutoka Moshi kwenda mikoa mbalimbali nchini, hususan Dar es Salaam, wameendelea kusota katika Stendi Kuu ya Mabasi Moshi kutokana na mgomo wa madereva unaoendelea nchini. Mwananchi limefika stendi hiyo leo Septemba 30, 2026 na kushuhudia mabasi machache yakiwa kituoni, huku baadhi ya abiria wakisema wamekwama tangu jana kutokana na kukosekana kwa usafiri.
Mmoja wa abiria, January Kateri, amesema alishindwa kusafiri jana baada ya kukosa basi na kulazimika kurudi nyumbani, huku leo akirejea stendi akitumaini kupata usafiri wa kwenda Dar es Salaam. Amesema mgomo huo umemvurugia mipango yake na kuitaka Serikali kutafuta suluhisho la haraka ili wananchi wanaotegemea usafiri wa umma wasiendelee kuathirika.
Kwa upande wao, baadhi ya madereva waliokuwapo stendi hiyo wamesema hawawezi kuanza safari hadi watakapopata maelekezo kutoka kwa viongozi wao. Dereva wa basi la Kapricon, Doto Jumanne, amesema hawajaridhishwa na maelezo yaliyotolewa na W...
- Title
- VIKOSI VYAONGEZWA KUDHIBITI MOTO MLIMA KILIMANJARO
- Runtime
- 4:46
- Date posted
- 3 days ago
- Description
- Siha. Serikali imeongeza vikosi vya kukabiliana na moto unaoendelea katika maeneo ya Shira 1 na Shira 2 ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA), mkoani Kilimanjaro, huku zaidi ya askari 135 wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiwa mlimani kushiriki katika operesheni hiyo.
Akikagua mwenendo wa zoezi la kuzima moto huo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamad Hassan Chande, amesema hatua hiyo imechukuliwa kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya moto huo, huku Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likishirikiana na maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Chande amepongeza uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa ushirikiano unaotolewa katika operesheni hiyo, akisema Mkuu wa Mkoa Nurdin Babu amekuwa akiratibu hatua za kuongeza nguvu, ikiwemo kumtuma Mkuu wa Wilaya ya Siha, Christopher Timbuka, pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama kushiriki katika zoezi hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Siha, Timbuka, amesema mbali na vyombo vya ulinzi na usalama...
- Title
- Mgomo wa madereva waendelea, abiria wadai nauli
- Runtime
- 3:01
- Date posted
- 3 days ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- MGOMO WA MADEREVA, POLISI WAIMARISHA ULINZI
- Runtime
- 0:36
- Date posted
- 3 days ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- MGOMO WA MADEREVA WAINGIA SIKU YA PILI STENDI YA MAGUFULI
- Runtime
- 2:31
- Date posted
- 3 days ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- Abiria waendelea kusota stendi ya Magufuli, safari zahamishiwa kesho
- Runtime
- 1:24
- Date posted
- 3 days ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- Waziri Katambi alivyowasili Magufuli kuzungumza na madereva
- Runtime
- 1:57
- Date posted
- 4 days ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- Polisi wang'oa namba za magari, madereva waliogoma kuondoa mabasi Stendi Magufuli
- Runtime
- 1:21
- Date posted
- 4 days ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- INSIDE THE MIND OF AN AFRICAN FINTECH VETERAN
- Runtime
- 28:22
- Date posted
- 4 days ago
- Description
- We sat down with one of Africa’s best-known fintech leaders, Sitoyo Lopokoiyit, the Chief Executive: Personal and Private Banking at Absa Group during his visit to Tanzania for a wide-ranging conversation on the country's growth story, digital adoption and acceleration, the future of financial services, and the advantages of building businesses with a Pan-African perspective.
- Title
- Msando aagiza madereva kuondoa mabasi Stendi ya Magufuli
- Runtime
- 1:45
- Date posted
- 4 days ago
- Description
- Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando amewataka madereva kuondoa mabasi yao katika Stendi ya Magufuli jijini Dar es Salaam, akisema muda wa kuyahifadhi mabasi hayo ndani ya stendi hiyo umeisha.
Msando ametoa kauli hiyo leo Septemba 29, 2026 kutokana na mgomo wa madereva katika Stendi ya Magufuli na maeneo mengine nchini, unaohusishwa na kupinga mfumo mpya wa Jeshi la Polisi, Kitengo cha Usalama Barabarani, wa kukata pointi kwenye leseni za udereva kwa madereva wanaokiuka sheria za barabarani.
Madereva hao wanapinga utaratibu huo wakidai kuwa baadhi ya makosa yanayoweza kusababisha kukatwa pointi, ikiwamo kutumia tairi mbovu au kuendesha gari lenye hitilafu, yanapaswa kumhusisha zaidi mmiliki au mwajiri wa gari kuliko dereva.
Akizungumza kuhusu hali hiyo, Msando amesisitiza kuwa Stendi ya Magufuli ni kwa ajili ya shughuli za usafirishaji na siyo eneo la kuhifadhi mabasi, akisema, “Stendi sio yadi.”
- Title
- MGOMO WA MADEREVA WATIKISA MOSHI
- Runtime
- 4:09
- Date posted
- 4 days ago
- Description
- Madereva wa mabasi yaendayo mikoa mbalimbali nchini wamegoma kwa saa kadhaa katika Stendi Kuu ya Mabasi Moshi, mkoani Kilimanjaro, wakipinga utaratibu wa kukatwa alama za makosa ya barabarani baada ya kutozwa faini.
Madereva hao wamesema utaratibu huo unawaweka katika adhabu mbili kwa kosa moja, wakieleza kuwa dereva anapotozwa faini ya Sh30,000 kwa kosa la barabarani, hapaswi pia kupunguziwa alama kwenye leseni yake kwa kosa hilo hilo. Hali hiyo ilisababisha baadhi ya mabasi kushindwa kuendelea na safari na kuwaacha abiria wakisubiri kituoni.
Akizungumza na Mwananchi leo Septemba 29, 2026, dereva wa basi la Masalu, Shedrack Kaaya, amesema mfumo huo umeongeza mzigo kwa madereva na unaweza kuhatarisha ajira zao endapo alama kwenye leseni zao zitapungua kutokana na makosa wanayodai tayari wameyalipia kwa faini. Naye dereva wa mabasi ya Lim Safari, Emanuel Singine, amesema madereva wamekuwa wakibeba mzigo mkubwa wa adhabu, hata katika baadhi ya makosa yanayohusis...
- Title
- HALI ILIVYO STENDI YA MAGUFULI MADEREVA WA MABASI WAGOMA
- Runtime
- 1:11
- Date posted
- 4 days ago
- Description
- Hali ilivyo katika Stendi ya Magufuli Mbezi jijini Dar es Salaam leo Septemba 29, 2026, ambapo madereva wa mabasi yaendayo mikoani wamegoma, wakipinga mfumo mpya wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani kukata pointi kwenye leseni za udereva wanapofanya makosa ya barabarani.
Chini ya utaratibu huo unaotokana na Tangazo la Serikali Na. 420 (G.N. No. 420), kila leseni ya udereva ina pointi 15, ambazo hupunguzwa kulingana na aina na uzito wa kosa la usalama barabarani linalofanywa na dereva.
Madereva hao wanadai kuwa baadhi ya makosa, ikiwamo kutumia tairi mbovu au kuendesha gari lenye hitilafu, yanapaswa kuwajibisha mmiliki au mwajiri wa gari badala ya dereva kukatwa pointi kwenye leseni yake.
- Title
- SAA 24 ZA MOTO MACHINGA UBUNGO KUONDOKA /HATUJUI TWENDE WAPI/CHALAMILA ATOA AGIZO KALI
- Runtime
- 3:28
- Date posted
- 5 days ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- "WENYE HATIA NDIO WAOGA..." KAULI YA MWISHO YA LISSU KUHUSU KESI YA UHAINI YAWAGUSA WAFUASI CHADEMA
- Runtime
- 3:27
- Date posted
- 5 days ago
- Description
- Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, leo Jumatatu, Septemba 28, 2026 amehitimisha kuwasilisha hoja zake za mwisho katika kesi ya uhaini inayomkabili, akiishawishi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imuone hana hatia na kumuachia huru.
Amewataka wanachama na wafuasi wa chama chake, Chadema kutokuwa na hofu kwani watashinda, akisema watu wenye hatia ndiyo wanaopaswa kuogopa.
"Mtashinda, msiogope, watu wenye hatia ndio huwa wanaogopa, wenye hatia ndio waoga, wana hofu, nyie mna hofu gani? mna hatia gani?” amesema Lissu baada ya kesi kuahirishwa wakati akitoka katika chumba cha Mahakama hiyo.
Lissu ametoa kauli hiyo kwa wafuasi wake leo Jumatatu, Septemba 28, 2026, muda mfupi baada ya kesi yake
kuahirishwa, kabla ya kushuka kutoka kizimbani.
Lissu ambaye pia ni wakili, anakabiliwa na kesi ya uhaini akidaiwa kutenda kosa la kuitishia Serikali, kin...
- Title
- TANZANIA INAVYOSAKA AJIRA NJE, YAJIPANGA DOHA DIALOGUE OKTOBA
- Runtime
- 16:45
- Date posted
- 5 days ago
- Description
- Wakati ukosefu wa ajira ukiendelea kuwa changamoto kwa vijana na wahitimu, Serikali imepanua wigo wa kutafuta fursa za ajira nje ya nchi, ikisema Watanzania 15,717 wamepata ajira katika mataifa mbalimbali ndani ya miaka miwili.
Serikali pia imesema Watanzania 8,804 wameunganishwa na fursa za ajira kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu, huku ikiendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha uhamaji wa nguvu kazi unafanyika kwa usalama na kuzingatia haki za wafanyakazi.
Kauli hiyo ilitolewa leo, Jumatatu, Septemba 28, 2026, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano wa pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, utakaofanyika Dar es Salaam Oktoba 5 na 6.
Mkutano huo utawakutanisha wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba (GCC), Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar, Kuwait, Oman na ...
- Title
- Dawasa yaweka uangalizi maeneo 20 kukabili El- Nino
- Runtime
- 13:40
- Date posted
- 5 days ago
- Description
- Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) imeweka uangalizi maalumu katika maeneo 20 ya miundombinu ya maji ili kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El- Nino.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mkama Bwire, amesema maeneo hayo yanahusisha vyanzo vya maji, mitambo ya uzalishaji, mabomba makubwa ya kusafirisha maji na mifumo ya majitaka.
Amesema mamlaka hiyo imefanya tathmini kubaini maeneo yenye hatari kubwa ya mafuriko na mmomonyoko wa ardhi, huku hatua za kuimarisha kingo za mito na kulinda mabomba zikichukuliwa.
Bwire amesema maeneo ya Mto Mpiji, Selander Bridge na Jangwani ni miongoni mwa maeneo yanayopewa uangalizi kutokana na historia ya kuathiriwa na mafuriko.
Amesema Dawasa pia imeweka vifaa vya dharura, ikiwamo mabomba ya maji ili kurahisisha urejeshaji wa huduma endapo miundombinu itaharibika.
- Title
- ASKOFU MWAMAKULA AMUOMBEA LISSU AKIHITIMISHA HOJA ZA MWISHO KUJINASUA KESI YA UHAINI
- Runtime
- 5:56
- Date posted
- 5 days ago
- Description
- Askofu Emmaus Mwamakula pamoja na Mchungaji Rose Masesa, dada mkubwa wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, wameongoza maombi kwa wafuasi wa chama hicho kwa ajili ya kumuombea Lissu.
Maombi hayo yamefanyika leo, Jumatatu, Septemba 28, 2026, kabla ya Lissu kupanda kizimbani katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kuendelea na majumuisho ya mwisho katika kesi ya uhaini inayomkabili.
Lissu tayari amepanda kizimbani kuwasilisha hoja ya nane na ya tisa, akilenga kuishawishi Mahakama kwamba hana hatia katika mashtaka yanayomkabili
- Title
- DAKTARI AFAFANUA MATESO WANAYOPITIA WENYE SIKOSELI, WENYE VINASABA WAPO KWENYE MAHUSIANO KUACHANA?
- Runtime
- 17:58
- Date posted
- 6 days ago
- Description
- Utafiti mpya umebaini kuwa kati ya asilimia 15 na 23 ya wanafunzi waliopimwa katika mikoa 13 nchini wana kinasaba kimoja cha selimundu maarufu sikoseli, hali iliyowasukuma wataalamu kutaka upimaji uanze mapema kwa watoto.
Wakati utafiti ukija na matokeo hayo, watoto wanaozaliwa na sikoseli pia idadi yao inaongezeka kutoka 9000 kwa mwaka 2019 hadi 14,000 mwaka 2025.
Wataalamu wanasema mtu mwenye kinasaba hicho anaweza kuishi maisha ya kawaida bila dalili, lakini akawa na uwezekano wa kumzaa mtoto mwenye ugonjwa huo endapo mwenza wake pia ana kinasaba kinachosababisha sikoseli.
Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa Mtandao wa Wadau Wanaoshughulika na Ugonjwa wa Sikoseli Tanzania (TSDA), Dk Elisha Osati, amependekeza upimaji uingizwe katika huduma za kawaida za afya, ikiwemo kliniki za chanjo.
Akizungumza na Mwananchi Septemba 21, 2026, Dk Osati amesema lengo ni kumwezesha mtoto kufahamu hali yake mapema na kupata elimu kadri anavyokua, k...
- Title
- CCM IRINGA YAMFUTA KAZI KATIBU WAKE GOHA, SABABU YA MAADILI YATAJWA
- Runtime
- 3:53
- Date posted
- 7 days ago
- Description
- Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Said Goha, amefutwa kazi na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Idara ya Oganaizesheni, Paul Chacha, kwa tuhuma za maadili ikidaiwa kuchafua taswira ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Uamuzi huo umetolewa leo Septemba 26, 2026, na Chacha wakati akizungumza katika mkutano maalumu wa CCM Mkoa wa Iringa uliohusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa CCM na Jumuiya zake mwaka 2027, pamoja na maandalizi ya maadhimisho ya miaka 50 ya chama hicho.
Chacha amesema Goha hatavuliwa majukumu ndani ya chama, bali atapangiwa jukumu jingine, huku CCM ikianza mchakato wa kumpata Katibu mpya wa Mkoa wa Iringa. Amesema kwa kipindi hiki, chama kitaendelea kuongozwa na Katibu mwingine hadi atakapopatikana atakayeziba nafasi hiyo.
Amesisitiza kuwa CCM haitamfumbia macho kiongozi au mwanachama ambaye mwenendo wake unaathiri taswira ya chama, akisisitiza umuhimu wa nidhamu na kulinda heshima ya CCM.
- Title
- WAFANYABIASHARA RANGI TATU WALIA MALIPO YA MEZA, SERIKALI YAFAFANUA
- Runtime
- 8:21
- Date posted
- 7 days ago
- Description
- Wafanyabiashara katika eneo la Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam, wamelalamikia utaratibu mpya wa upangaji wa maeneo ya biashara katika soko hilo wakidai umeongeza gharama za uendeshaji wa biashara zao, huku wakilazimika kutozwa Sh200,000 kununua meza moja.
Wafanyabiashara hao waliovunjiwa vibanda vyao vya awali sokoni hapo, wamesema licha ya kutoa kiasi hicho cha fedha kununua meza, lakini thamani yake wanaona haiendani na kiasi wanachotozwa.
Wamedai meza walizopewa ni vipande vya bomba za chuma, ambazo wao wenyewe ndiyo wanatakiwa kuziboresha kwa kuzijemga nje ya kiasi cha Sh 200,000 walicholipishwa kila mmoja
Mbali na fedha hizo za meza, wamesema pia wanatakiwa kulipa Sh30,000 kama kodi ya mwezi pamoja na ushuru wa kila siku Sh1,000 hali wanayodai imekuwa mzigo kwao kutokana na kipato wanachoingiza.
- Title
- AWESO ATOA SIKU 30 MRADI WA MAJI WA KIMKAKATI WA NYANGAO - RUANGWA UKAMILIKE
- Runtime
- 4:53
- Date posted
- 7 days ago
- Description
- Lindi. Waziri wa Maji,Jumaa Aweso, amemuagiza Mkurugenzi anayesimamia miradi ya maji kuhakikisha anasimamia kwa karibu utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Kimkakati wa Nyangao - Ruangwa, ndani ya siku 30 wananchi wa vijiji 56 vya Wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Lindi waanze kunufaika na huduma hiyo ya maji.
Aweso ametoa agizo hilo Jana Ijumaa Septemba 25, 2026, katika maeneo ya Nanganga, Ruangwa na Mtama, mkoani Lindi, wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji mkoani humo
Mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Sh119bilioni unaolenga kuwanufaisha wananchi 123,657 katika vijiji 56, ambavyo ni vijiji 34 vya Ruangwa, 21 vya Nachingwea na kijiji kimoja Halmashauri ya Mtama.
Mradi huo unatumia chanzo cha Mto Nyangao (Chiuwe), chenye uwezo wa kuzalisha takribani lita milioni 14.3 za maji kwa siku, ikilinganishwa na mahitaji ya takribani lita milioni 9 kwa siku.
Naye Meneja wa RUWASA Mkoa wa Lindi, Mhandisi Muhi...
- Title
- CHALAMILA: FAMILIA YA MZEE AMEIR WANA UPENDO, HAWANA VITISHO, MAJIGAMBO | DAR IKIWA SAFI SITOFUKUZWA
- Runtime
- 7:28
- Date posted
- 7 days ago
- Description
- Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema atamkumbuka hayati Hafidh Ameir Hassan kwa namna alivyokuwa mpole na mtu wa kawaida licha ya kuwa mume wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisisitiza anamuombea dua ili roho yake Mungu aihifadhi mahali pema peponi.
"Tunamuenzi Ameir kwa malezi makubwa kwa familia yake, inayoishi maisha ya kawaida kwa upendo, hili ni jambo kubwa ambalo tunayaenzi maisha ya Mzee Ameir," amesema Chalamila.
Chalamila ameyasema hayo leo Septemba 26, 2026 katika Hitma iliyofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee imehudhuriwa na masheikh, maaskofu, wachungaji, mawaziri, manaibu waziri na wakuu wa taasisi, viongozi 12 wa vyama vya siasa na mabalozi wa Uturuki, Comoro, UAE, Yemen, Syria na Misri.
Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026 katika Hospitali ya Kumbumbuku ya Mzena, Zanzibar alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.
- Title
- BALAA LA KIFUNGU NA IBARA KUNDI LA VIJANA LINALORUDISHA UTAMADUNI/WANAJUA KUPIKA KILA KITU
- Runtime
- 31:32
- Date posted
- 7 days ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- “TUJIANDAE NA KIFO…’ MUFTI ASEMA TUTENDE YANAYOMPENDEZA MUNGU
- Runtime
- 6:18
- Date posted
- 7 days ago
- Description
- Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amewataka Waislamu kujiandaa na safari ya ahera, ambayo kila mmoja atakwenda, hivyo wanapaswa kufanya matendo mema yanayompendeza na kumridhisha Mwenyezi Mungu.
Sheikh Zubeir ameeleza hayo leo Jumamosi Septemba 26, 2026 katika hitima ya kumuombea aliyekuwa mume wa Rais Samia Suluhu Hassan, hayati Hafidh Ameir Hassan iliyoandaliwa na familia ya Ameir iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Hitima hiyo imefanyika ukumbi wa Diamond imehudhuriwa na masheikh, maaskofu, wachungaji, mawaziri, manaibu waziri na wakuu wa taasisi, viongozi 12 wa vyama vya siasa na mabalozi wa Uturuki, Comoro, UAE, Yemen, Syria na Misri.
Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026 katika Hospitali ya Kumbumbuku ya Mzena, Zanzibar alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Amesisiza Waislamu na Watanzania kujiandaa na safari ya kifo kwa kuhakikisha wanatenda au kufanya mambo mema na siyo yanayomchukiza Mwenyezi ...
- Title
- MKUMBAVANA: MWAMBA WA MAUTI ULIOBEBA SIRI ZA WAPARE
- Runtime
- 8:05
- Date posted
- 7 days ago
- Description
- Kwa miaka mingi, mwamba wa Mkumbavana uliopo katika maeneo ya milima ya Wilaya ya Mwanga, Kilimanjaro, umebeba simulizi nzito za Wapare kuhusu mila iliyowahi kuhusisha kuwaondoa katika jamii watoto walioaminika kuwa na “mkosi” kutokana na namna walivyozaliwa.
Simulizi za wazee wa jamii hiyo zinaeleza kuwa mwanzoni mwa miaka ya 1900, baadhi ya watoto waliokuwa wakianza kuota meno ya juu kabla ya ya chini au waliozaliwa wakiwa na vidole sita walihusishwa na imani hizo na kupelekwa Mkumbavana, ambako waliangaliwa kwa utaratibu wa kimila kabla ya kuachwa kwenye eneo lenye miamba na maporomoko makali.
Kwa mujibu wa wazee hao, mtoto aliyefikishwa katika eneo hilo alikuwa akipewa chakula na kunyonyeshwa kwa mara ya mwisho na mama yake kabla ya kulazwa kwenye mwamba huo akiwa amelala. Wazazi waliondoka bila kurudi nyuma, huku mtoto akiachwa kukabiliana na mazingira hatari ya eneo hilo.
Mzee Matata Marijani, mkazi wa Mbambua Juu, anasema utaratibu huo ...
- Title
- KAYA ZENYE MIFUMO MIBOVU UKUSANYAJI TAKA KUKIONA CHA MOTO
- Runtime
- 2:14
- Date posted
- 7 days ago
- Description
- Serikali yaanza kuzichukulia hatua za kisheria kaya zenye mifumo mibovu ya ukusanyaji wa taka na mitaro ya maji taka.
Zoezi la usafishaji wa mitaro ya maji na usafi wa mazingira mkoani shinyanga linalolenga kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na mvua za el ino limevaa sura mpya baada ya Mkuu wa mkoa Mboni Mhita kuagiza kaya zote zenye mifumo mibovu ya ukusanyaji wa taka na mitaro michafu ya maji taka kuchukua hatua kali za kisheria ikiwemo kupigwa faini.
Maelekezo hayo yametolewa leo Septemba 26, 2026 na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita katika uzinduzi wa kampeni ya utekelejani wa agizo la serikali la usafi wa mazingira akisisitiza wamkuu wa wilaya, wenyeviti wa vijiji na mitaa kuendeleza mikakati ya kutoa elimu kwa umma juu ya usafi wa mazingira.
Akipokea maelekezo hayo mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro ameeleza utayari wa viongozi na wananchi katika kuhakikisha maekekezo ya serikali yanafuatwa.
Nao baadhi ya wanan...
- Title
- MC GARA B, ALIVYOIPENDA SIMBA
- Runtime
- 4:29
- Date posted
- 7 days ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- KILICHOJIFICHA MTOTO WA MCHUNGAJI CHINI YA DARAJA LA KIJAZI.
- Runtime
- 14:26
- Date posted
- 8 days ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- KILICHOJIFICHA MTOTO WA MCHUNGAJI CHINI YA DARAJA LA KIJAZI.
- Runtime
- 20:19
- Date posted
- 8 days ago
- Description
- Mwanangu alikuwa ana hamu sana ya kumwona baba yake tangu akiwa mdogo. Lakini alipoenda kule, ushirikiano ukawa mdogo na mama wa kambo hakuwa na ukaribu naye.
“Hata nauli ya kwenda shule alikuwa anakatwa, mtoto akawa hapati hata hela ya kula shuleni. Ni kweli alikuwa na changamoto za udokozi zilizotokana na tamaa za kitoto na ukosefu wa malezi ya pamoja, lakini mimi kama mama bado naumia kuona maisha anayoishi,” amesema mama huyo.
Baba akanusha akidai amepata fursa nyingi
Kwa upande wake, baba yake Cyprian anayejulikana kwa jina la Daud John, ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Mlima Sinai, maarufu kwa jina la Pastor Debe, anayeishi Salasala Mbuyuni, amekanusha madai ya mwanawe.
- Title
- KILICHOJIFICHA MTOTO WA MCHUNGAJI CHINI YA DARAJA LA KIJAZI.
- Runtime
- 27:00
- Date posted
- 8 days ago
- Description
- “Naahidi kama nikipata msaada huo nitatoka mtaani. Natamani nirudi shule na nitapambana ili nitoke kwenye haya maisha,” anasema kijana huyo huku akilengwa na chozi.
Safari iliyokatizwa
Akizungumza na Mwananchi hivi karibuni, Cyprian amesema aliwahi kupata fursa ya kusoma kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kupitia kituo cha kulelea watoto cha Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Korogwe. Safari yake ya elimu ilisimama baada ya kufeli mtihani wa kidato cha nne (QT).
“Kwenye mtihani wa kidato cha nne, kwa bahati mbaya nilifeli. Baada ya hapo viongozi wa kituo wakasema sitakiwi kukaa pale kwa sababu nimefeli.”
“Nilijaribu kwenda kuomba msamaha na kufuatilia barua Ustawi wa Jamii, lakini ilikuwa mzunguko mkubwa. Mimi ndoto yangu bado ipo shuleni. Natamani niwe mwanasheria ili nije kuwatetea wenzangu mtaani ambao wengi wao wanasingiziwa kesi na kukosa wa kuwatetea,” amesema.
Amesema baada ya hapo, changamoto za kifamilia zilizidi kumwe...
- Title
- KILICHOJIFICHA MTOTO WA MCHUNGAJI CHINI YA DARAJA LA KIJAZI.
- Runtime
- 20:44
- Date posted
- 8 days ago
- Description
- Dar es Salaam. Kijana Cyprian Daud (17) amekuwa akiendesha maisha yake kwa kufuta vioo vya magari vioo na kujipatia ujira ili kuendesha maisha. Simulizi ya mtoto huyo ina pande mbili hadi kufikia hatua ya kujikuta katika safari hiyo ya maisha kutokana na maisha aliyoyapitia, huku baba mzazi ambaye ni mchungaji akieleza kwa kina nini kimesababisha hadi kujikuta katika maisha hayo.
Ni maisha ambayo hakuyapanga. Chini ya daraja hilo amefanya makazi kwa takribani miezi minane baada ya kurejea kutoka mkoani Iringa. Hata hivyo, licha ya mazingira hayo, kijana huyo bado anashikilia ndoto yake ya kusoma na kuwa mwanasheria.
Anasema anataka kutumia taaluma hiyo kuwatetea watoto wengine wanaoishi katika mazingira magumu ya mitaani ambao, kwa mtazamo wake, wengi hukosa watu wa kuwasimamia wanapokumbana na matatizo ya kisheria.
- Title
- MKUMBAVANA: MWAMBA WA MAUTI ULIOBEBA SIRI ZA WAPARE
- Runtime
- 8:05
- Date posted
- 8 days ago
- Description
- Kwa miaka mingi, mwamba wa Mkumbavana uliopo katika maeneo ya milima ya Wilaya ya Mwanga, Kilimanjaro, umebeba simulizi nzito za Wapare kuhusu mila iliyowahi kuhusisha kuwaondoa katika jamii watoto walioaminika kuwa na “mkosi” kutokana na namna walivyozaliwa.
Simulizi za wazee wa jamii hiyo zinaeleza kuwa mwanzoni mwa miaka ya 1900, baadhi ya watoto waliokuwa wakianza kuota meno ya juu kabla ya ya chini au waliozaliwa wakiwa na vidole sita walihusishwa na imani hizo na kupelekwa Mkumbavana, ambako waliangaliwa kwa utaratibu wa kimila kabla ya kuachwa kwenye eneo lenye miamba na maporomoko makali.
Kwa mujibu wa wazee hao, mtoto aliyefikishwa katika eneo hilo alikuwa akipewa chakula na kunyonyeshwa kwa mara ya mwisho na mama yake kabla ya kulazwa kwenye mwamba huo akiwa amelala. Wazazi waliondoka bila kurudi nyuma, huku mtoto akiachwa kukabiliana na mazingira hatari ya eneo hilo.
Mzee Matata Marijani, mkazi wa Mbambua Juu, anasema utaratibu huo ...
- Title
- WAFANYABIASHARA RANGI TATU WALIA MALIPO YA MEZA, SERIKALI YAFAFANUA
- Runtime
- 6:23
- Date posted
- 8 days ago
- Description
- WAFANYABIASHARA RANGI TATU WALIA MALIPO YA MEZA, SERIKALI YAFAFANUA
- Title
- KONGAMANO LA FURSA NA UWEKEZAJI USHIRIKI WA SEKTA BINAFSI KWENYE PPP
- Runtime
- 3:33:05
- Date posted
- 8 days ago
- Description
- KONGAMANO LA FURSA NA UWEKEZAJI USHIRIKI WA SEKTA BINAFSI KWENYE PPP
- Title
- KONGAMANO LA FURSA NA UWEKEZAJI USHIRIKI WA SEKTA BINAFSI KWENYE PPP
- Runtime
- 0:00
- Date posted
- 8 days ago
- Description
- KONGAMANO LA FURSA NA UWEKEZAJI USHIRIKI WA SEKTA BINAFSI KWENYE PPP

