Mwananchi Digital
KITILA: UKUAJI WA UCHUMI UENDANE NA KIWANGO CHA KUPUNGUZA UMASKINI NA KUZALISHA AJIRA
- Title
- KITILA: UKUAJI WA UCHUMI UENDANE NA KIWANGO CHA KUPUNGUZA UMASKINI NA KUZALISHA AJIRA
- Runtime
- 5:21
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Tume ya Taifa ya Mipango, inayoongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, imejadili mwongozo wa kitaifa wa ufuatiliaji na tathimini ya miradi ya maendeleo na kuidhinisha maeneo makuu matatu ya kimkakati yanayohitaji mageuzi makubwa.
Maeneo hayo ni mageuzi katika mifumo ya utawala wa utumishi wa umma, ambayo yanajumuisha viashiria vya upimaji 13; mageuzi katika uwekezaji na uzalishaji, yenye viashiria vya upimaji 53 na mageuzi katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na mazingira, ambayo yatajikita zaidi katika kuboresha utoaji wa huduma.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, aliposisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha utekelezaji wa mipango ya sasa unaenda sambamba na ukuaji wa uchumi, kupunguza umaskini na kuongeza ajira nchini.
Amezungumza hayo katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unaoend...
- Title
- MAGORI: CHAMA HAKUPENDA KWENDA YANGA
- Runtime
- 5:37
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- MALISA ASIMULIA MAFUNZO, MACHUNGU YA SIKU 183 ALIZOKAA GEREZANI
- Runtime
- 6:59
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Moshi. Zikiwa zimepita siku tisa tangu alipoachiwa huru, Mchungaji Godfrey Malisa amesema kipindi cha siku 183 alizokaa gerezani kilikuwa chuo cha mafunzo, huku akishauri kufanyika kwa marekebisho katika mfumo wa utoaji msamaha kwa wafungwa ili uwaguse wengi zaidi.
Malisa alisema akiwa huko alikutana na wafungwa waliokaa magerezani kwa muda mrefu, baadhi yao kwa miaka 15 hadi 18, huku wengine wakiwa ni watu wenye ulemavu ambao huendelea kuwa na matumaini tasa kila misamaha inapokuwa ikitangazwa.
Hata hivyo, alisema mara nyingi misamaha hiyo haiwagusi wafungwa hao, jambo ambalo huwasababishia maumivu makubwa na kukata tamaa.
Ametoa kauli hiyo katika mahojiano maalumu na Mwananchi Digital, siku tisa baada ya kuachiwa huru kufuatia kukabiliwa na mashtaka mbalimbali, likiwamo la uhaini, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.
Hii ni sehemu ya kwanza usikose sehemu ya pili.
- Title
- BABA LEVO AFAFANUA UJAUZITO WA ZUCHU, MAISHA YA SIASA, MUZIKI & UCHAWA KUACHIA NGOMA MPYA NA DIAMOND
- Runtime
- 13:53
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Clayton Chipando maarufu kama Baba Levo, amesema bado anaiona tasnia ya muziki kuwa sehemu kubwa ya maisha yake licha ya kuingia kwenye siasa kwa kuwawakilisha wananchi bungeni.
Msanii huyo ambaye aliwahi kutamba na nyimbo kama ‘Amen’, ‘Amapiano’ na nyinginezo, alisema nafasi yake ya ubunge imekuwa daraja muhimu la kuwasemea wasanii moja kwa moja serikalini.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi Digital, Baba Levo amesema moja ya vitu anavyojivunia ni uwezo wake wa kuielewa sanaa kwa undani kutokana na maisha aliyopitia kwenye muziki kabla ya kuwa mbunge. Kwa mujibu wake, changamoto nyingi zinazowakabili wasanii zinaweza kutatuliwa kwa haraka iwapo zitafikishwa kwenye mamlaka husika kwa njia sahihi.
Hii ni sehemu ya kwanza usikose sehemu ya pili.
- Title
- SHUHUDIA MAZISHI YA MAMA MAGUFULI
- Runtime
- 1:57
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Haya ndio mazishi ya Mama Sussana, mama mzazi wa Hayati Dk John Magufuli, yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu wilayani Chato mkoani Geita jana Mei 29, 2026.
- Title
- DK NCHIMBI AWATAKA WAZAZI KUMUENZI MAMA MAGUFULI KWA MALEZI BORA
- Runtime
- 2:58
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Emmanuel Nchimbi amewataka wazazi na walezi nchini kuiga mfano wa malezi bora ya marehemu Sussana Ngolo kwa kuhakikisha wanalea watoto wenye maadili na uwezo wa kulitumikia taifa.
Dk Nchimbi ametoa kauli hiyo leo Ijumaa, Mei 29, 2026 alipomwakilisha Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Mama Sussana, mama mzazi wa Hayati Dk John Magufuli, yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu wilayani Chato mkoani Geita.
Amesema Mama Sussana, licha ya kutokuwa katika familia ya kisiasa, alitimiza wajibu wake wa malezi na hivyo kusaidia taifa kupata kiongozi mahiri na mchapakazi.
“Wazazi wana wajibu wa kulea watoto kwa kuwaandaa kulitumikia taifa. Kufanya mema kwa binadamu mwenzako siyo lazima yalipwe kwako,” amesema.
Dk Nchimbi amesema kutokana na malezi hayo, Hayati Rais Magufuli aliendeleza fikra za kulea na kuandaa viongozi wengine, akitolea mfano msaada wake wakati wa mabadiliko yake ...
- Title
- MSIGWA APOKELEWA RASMI CHADEMA, ASEMA AJENDA NI KUTETEA WANANCHI
- Runtime
- 3:17
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Iringa. Aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mchungaji Peter Msigwa, amepokewa rasmi kurejea katika chama chake cha zamani cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Jimbo la Iringa Mjini.
Hafla ya mapokezi hayo imefanyika katika ofisi za Chadema jimbo zilizopo Veta, Manispaa ya Iringa na imehudhuriwa na viongozi mbalimbali, wanachama na wafuasi wa chama hicho.
Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Msigwa amesema kuwa ameamua kurejea Chadema kwa lengo la kuendelea kupigania haki za msingi za wananchi na kutetea ustawi wao na kuwa bado kuna changamoto nyingi zinazowakabili Watanzania. Hivyo anaamini kupitia chama hicho ataweza kushiriki kikamilifu katika kutafuta suluhisho la matatizo hayo.
Aidha, Msigwa amewataka wanachama wa Chadema kuendelea kujenga hoja zenye mashiko na zinazogusa maisha halisi ya wananchi na amesisitiza umuhimu wa siasa zinazolenga maendeleo ya jamii, mshikamano na ustawi wa wananchi.
- Title
- 78 MBARONI, SILAHA MOJA YAKAMATWA, SHINYANGA
- Runtime
- 3:37
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Shinyanga. Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga limekamata watuhumiwa 78 kwa makosa mbalimbali pamoja na silaha moja aina ya Bastola TISAS yenye namba za usajili T0620-22J00122 ikiwa na risasi 11, ililipotiwa kuibiwa Mei 10, 2026 katika mtaa wa Nyakato wilayani Kahama, ambapo ilikuwa kihalali ni mali ya Richard Mhabi (38) ambaye ni mfanyabiashara wa Kahama.
Akizungumza leo Mei 29, 2026 na vyombo vya habari wakati wa kutoa taarifa ya mwezi wa tano, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi ameeleza kuwa, pia wahamiaji haramu 11 kwa nyakati tofauti tofauti kwa kuishi ndani ya nchi bila kibali, pia limekamata vielelezo mbalimbali,
“Watuhumiwa 78 wamekamatwa kwa makosa mbalimbali, silaha moja aina ya Bastola TISAS yenye namba za usajili T0620-22J00122 ikiwa na risasi 11, sambamba vielelezo ikiwamo mafuta ya diseli lita 480, mabati 558, bangi kete 228, pombe ya moshi lita 115, mirungi kilogramu 89, pikipiki 11 pamoja na betri za gari 03” amesema M...
- Title
- SH21 MILIONI ZAREJESHWA TAKUKURU , SHINYANGA
- Runtime
- 3:07
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Shinyanga. Katika kipindi cha mwezi Januari – Machi 2026 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Shinyanga imeafnikiwa kurejesha kiasi cha Sh21,897,954 kutokana na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha, uchunguzi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jamii ikiwamo fedha kutokana na ushuru wa ujenzi wa shule kwa TRA.
Akizungumza leo Mei 29, 2026 na vyombo vya habari, Kamanda wa Takukuru mkoa wa Shinyanga Donasian Kessy ameeleza kuwa hatua hiyo imekuwa ni mafanikio yaliyotokana na uelimishaji wa jamii kwa njia ya semina mbalimbali zilizotolewa ambayo imesaidia kuongezeka kwa uadilifu,
“Kwa kipindi cha Januari hadi Machi, 2026 Sh21,897,954 zimerejeshwa kupitia ufuatiliaji wa matumizi wa fedha, ambapo Sh5,540,254 zimeokolewa kupitia ujenzi wa shule ya awali na msingi Tinde ‘B’, baada ya kubainika Sh5,316,304 ilipaswa kulipwa TRA ikiwa ni kodi na Sh223,950 ushuru wa huduma kwa Halmashauri ya Shinyanga, sambamba na kiasi cha Sh9,672,000 zime...
- Title
- Magori: Mauzo ya Ahoua, Kibu na Mukwala yalizaa kina Gueye na Oura
- Runtime
- 6:48
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Crescentius Magori amesema uamuzi wa kuwauza nyota wao watatu ndiyo siri ya kuwasajili nyota wanane walioboresha kikosi hicho katika dirisha dogo na kupata timu ya ushindani.
Akizungumza na Mwananchi Digital alipofanya ziara yake Kampuni ya Mwananchi, Tabata amesema hatua ya kutengeneza kikosi cha ushindani kinachoendelea kufanya vizuri haikuwa rahisi kutokana na kukosekana kwa bajeti ya kutosha.
Magori alisema Simba ilisajili wachezaji wanane katika dirisha dogo la Januari ambao ni kipa Djibril Kassali, mabeki Nickson Kibabage, Ismaila Toure, viungo Libasse Gueye, Anicet Oura, Inno Loemba, Clatous Chama na mshambuliaji Baraka Mwangosi hiyo ilitokana na fedha walizopata baada ya mauzo ya wachezaji wake watatu.
Januari wakati wa dirisha dogo Simba iliwauza, kiungo Jean Charles Ahoua aliyenunuliwa na CR Belouizdad ya Algeria, mshambuliaji Steven Mukwala na kiungo mshambuliaji Kibu Denis aliyeuza Al Nasri y...
- Title
- BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU, KIKAO CHA THELATHINI NA TISA TAREHE 29 MEI, 2026
- Runtime
- 4:33:49
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU, KIKAO CHA THELATHINI NA TISA TAREHE 29 MEI, 2026
- Title
- HAFLA YA KUHITIMISHA MAFUNZO YA MAAFISA NA WAKAGUZI WASAIDIZI WA JESHI LA POLISI
- Runtime
- 1:16:16
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- HAFLA YA KUHITIMISHA MAFUNZO YA MAAFISA NA WAKAGUZI WASAIDIZI WA JESHI LA POLISI
- Title
- HAFLA YA KUHITIMISHA MAFUNZO YA MAAFISA NA WAKAGUZI WASAIDIZI WA JESHI LA POLISI
- Runtime
- 2:33:11
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- HAFLA YA KUHITIMISHA MAFUNZO YA MAAFISA NA WAKAGUZI WASAIDIZI WA JESHI LA POLISI
- Title
- #live: SUSTAINABILITY, TRUST & GROWTH IN AFRICA
- Runtime
- 1:59:34
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- MTLF presents Bolt Tanzanian Mobility Dialogue 2026.
- Title
- TSHABALALA AFICHUA BATO LAKE NA BOKA, AMKUMBUKA IBRAHIM AJIBU, ANENA ALIVYO NA KIU YA MATAJI YANGA
- Runtime
- 12:44
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
#samiasuluhuhassan #simbasc #yangasc #mashabiki #nbcpremeireleague #cafchampionsleague #cafconfiderationcup #ikulumawasiliano #entertainment #music #news #yangasc #simbasc #cafchampionsleague #mayele #highlights #cafconfiderationcup #riversunited #mashabiki #yangaleo #yanga #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko #entertainment #music #news #magoliyasimba #magoliyayanga #magoliyote #magoliyamayele #mayele #aziziki #manara #manaraleo #ikulumawasiliano...
- Title
- MWALIMU AFUNGUKA UKARIBU WAKE NA SAMIA, SABABU KUUNGA MKONO MARIDHIANO, CHAUMMA CHAMA PROJECT
- Runtime
- 1:03:57
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi Digital.
- Title
- FAIZ ARAB ON TRUST, INNOVATION, AND TANZANIA'S BOOMING CAPITAL MARKETS
- Runtime
- 25:58
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Tanzania's financial sector is undergoing a transformation that few could have predicted just a decade ago. Capital markets, once considered the domain of institutional investors and wealthy individuals, are increasingly becoming a central part of the country's economic growth journey.
At the forefront of this evolution is iTrust Finance, a company that has transitioned from transaction advisory services to a major player in capital market investment and financial inclusion. In an exclusive interview with Mwananchi Communications Ltd, iTrust Finance CEO Faiz Arab provides insights into the company's journey, the opportunities and challenges facing Tanzania's capital markets, and the innovative solutions that are democratizing investment opportunities.
- Title
- MTOTO WA MIAKA MITATU ATEKETEA KWA MOTO MOSHI, MWILI WAKUTWA CHINI YA KITANDA
- Runtime
- 5:21
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Moshi. Simanzi na majonzi vimetawala katika Kitongoji cha Mwitini, Kijiji cha Mwasi Kusini wilayani Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro baada ya mtoto mwenye umri wa miaka mitatu, Francis Andrew David kufariki dunia kwa kuteketea kwa moto ndani ya nyumba yao.
Tukio hilo limetokea leo Mei 26, 2026 katika Kata ya Uru Mashariki, ambapo moto huo uliteketeza sehemu ya nyumba waliyokuwa wakiishi mtoto huyo pamoja na familia yake.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro,Jeremia Mkomagi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema chanzo cha moto bado kinachunguzwa.
Amesema Jeshi la Zimamoto lilipokea taarifa za tukio hilo majira ya saa 9:04 alasiri na askari walipofika eneo la tukio walikuta wananchi tayari wamefanikiwa kuuzima moto huo.
“Askari walikuta mwili wa mtoto Francis Andrew David ukiwa umeungua chini ya kitanda ndani ya nyumba hiyo, ndipo mwili huo ulikabidhiwa kwa Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi,”...
- Title
- Wenje: Ukawa ilisababisha mkwamo wa Katiba mpya
- Runtime
- 12:31
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU,KIKAO CHA THELATHINI NA SABA TAREHE 26 MEI, 2026
- Runtime
- 45:53
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU,KIKAO CHA THELATHINI NA SABA TAREHE 26 MEI, 2026
- Title
- LIVE: UAPISHO WA MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI TANZANI, UNAOFANYIKA IKULU JIJINI DAR ES SALAAAM
- Runtime
- 33:16
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- LIVE: UAPISHO WA MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI TANZANI, UNAOFANYIKA IKULU JIJINI DAR ES SALAAAM
- Title
- BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU,KIKAO CHA THELATHINI NA SABA MEI 26, 2026
- Runtime
- 43:18
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU,KIKAO CHA THELATHINI NA SITA MEI 25, 2026
- Title
- MAREKANI YAISHAMBULIA TENA IRAN, MLANGO WA HORMUZ WAZIDI KUCHEMKA.
- Runtime
- 3:14
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Washington. Marekani imesema imeanzisha mashambulizi mapya kusini mwa Iran, yaliyolenga maeneo ya makombora pamoja na boti zilizokuwa zikijaribu kuweka mabomu ya majini, katika eneo la Ghuba ya Uajemi, huku ikieleza hatua hiyo ilikuwa ya kujilinda na kulinda wanajeshi wake, dhidi ya vitisho vya vikosi, vya Iran.
Kwa mujibu wa Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM), mashambulizi hayo yalifanywa wakati ambapo Marekani inaendelea kudai kuwa inazingatia tahadhari, licha ya kuwepo kwa usitishaji wa mapigano unaoendelea kati yake na Iran, huku Msemaji wa CENTCOM, Kapteni Tim Hawkins alisema jeshi la Marekani litaendelea kujihami, dhidi ya vitisho vyovyote kutoka, Iran.
Mashambulizi hayo yaliripotiwa kulenga eneo karibu na Bandar Abbas, mji wa bandari uliopo kusini mwa Iran, ambao pia ni makazi ya kituo kikubwa, cha jeshi la wanamaji la Iran katika Mlango wa Hormuz, vyombo vya habari vya Iran vilisema mamlaka za eneo hilo zilianza uchunguzi baada ya milipuko kusi...
- Title
- NETANYAHU ATANGAZA VITA VIPYA DHIDI YA HEZBOLLAH, LEBANON
- Runtime
- 2:44
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Jerusalem. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema, taifa lake litaongeza mashambulizi dhidi ya kundi la Hezbollah nchini Lebanon, huku jeshi la Israel likitangaza kuanzisha mashambulizi mapya katika maeneo mbalimbali, ya nchi hiyo.
Jeshi la Israel (IDF) limesema limefanya mashambulizi katika Bonde la Bekaa mashariki mwa Lebanon, pamoja na maeneo mengine likidai kulenga ngome za Hezbollah, huku mashambulizi hayo yamekuja saa chache baada ya Netanyahu kutangaza kuwa, jeshi limepewa maelekezo ya kulipa kundi hilo, pigo kubwa.
Kundi la Hezbollah ambalo linaungwa mkono na Iran, limesema limejibu mashambulizi hayo kwa kufanya mashambulizi 22 ya droni, na makombora dhidi ya maeneo ya Israel huku kundi hilo likidai kulenga wanajeshi wa Israel, vifaru, kambi za kijeshi na majengo yaliyopo kaskazini, mwa Israel.
Mapema mwezi huu Israel na Lebanon zilikubaliana kuongeza muda wa usitishaji wa mapigano kwa siku 45, ingawa mapigano madogo yameendelea ...
- Title
- Wenje: Msigwa alinipigia simu kuniaga kwamba anarejea Chadema
- Runtime
- 7:29
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- HINJO: MPAKA SASA UBINGWA WA LIGI KUU NI MGUMU TUSUBIRI MECHI ZA MWISHO
- Runtime
- 5:31
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- Ngai: Hatuna presha Yanga tunajua namna ya kumalizia Ligi
- Runtime
- 2:15
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- KAMWE: AMPA NAFASI FEI TOTO KUWA MVP, ATOA TAHADHARI OKELLO MSIMFANANISHE NA CHAMA
- Runtime
- 9:28
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- Historia ya chumba cha Malkia ndani ya jengo la KNCU
- Runtime
- 2:04
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Moshi. Mwaka 1956, Princess Margaret, mdogo wake wa Malkia Elizabeth II, alifika mjini Moshi kama mwakilishi rasmi wa familia ya kifalme ya Uingereza katika sherehe za kumtawaza Mangi Mkuu wa Wachaga, Thomas Marealle. Ujio wake uliweka historia kubwa katika mji huo uliokuwa chini ya utawala wa kikoloni.
Wakati huo, Moshi ilijaa shamrashamra kubwa za mapokezi ya mgeni huyo wa hadhi ya juu, ambapo wananchi walijitokeza kwa wingi kushuhudia msafara wake ukipita kuelekea maeneo ya shughuli rasmi. Tukio hilo lilionekana kama moja ya matukio makubwa ya kifalme kuwahi kushuhudiwa Kilimanjaro.
Princess Margaret alifikia Hoteli ya KNCU iliyopo ndani ya jengo la Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Kahawa Kilimanjaro, ambako alilala katika chumba maalumu namba 10 kilichoandaliwa kwa heshima ya mgeni huyo wa kifalme. Hoteli hiyo ilikuwa miongoni mwa majengo ya kisasa zaidi Afrika Mashariki wakati huo.
KNCU ilijengwa kwa nguvu za wakulima wa kahawa walioun...
- Title
- Chalamila atoa kauli mchina aliyeuawa Dar
- Runtime
- 2:50
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amegusia tukio la mauaji raia wa china akisema kama marehemu angekuwa mwanasiasa anayejulikana waziwazi kwa chama fulani, kuna uwezekano watu wangeanza kutoa tafsiri za kisiasa mapema.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mei 25,2026 Chalamila amesema raia huyo wa China angekuwa anafahamika ni mwanachama wa chama fulani, watu wangesema ameuliwa kwa sababu ya itikadi yake lakini kwa kuwa hilo halipo, uchunguzi wake unaendelea katika mazingira ya kawaida.
Amewataka wananchi kuendelea kuwa na imani na vyombo vya usalama huku akisisitiza kuwa hali ya usalama katika Mkoa wa Dar es Salaam ipo shwari.
“Kwanza nitoe wasiwasi kwa wananchi wote kwamba hali ya usalama katika Mkoa wa Dar es Salaam ni nzuri sana. Pia niwasihi wawekezaji na wananchi wanaomiliki maeneo makubwa ya biashara hakikisheni mnatumia walinzi kutoka kampuni rasmi zilizosajiliwa na Serikali badala ya kuajiri watu binafsi,” amesema.
- Title
- SHAMBULIZI LA KIKATILI LAWAACHIA PAKISTAN SIMANZI KUBWA
- Runtime
- 2:51
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Pakistan. Takribani watu 20 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa, baada ya mlipuko mkubwa kulenga treni iliyokuwa ikisafirisha wanajeshi na familia zao nchini Pakistan, tukio hilo lilitokea katika kituo cha reli cha Chaman Phatak mjini Quetta, mji mkuu wa jimbo la Balochistan magharibi, mwa nchi hiyo.
Maofisa wa reli wameeleza kuwa, mabehewa matatu pamoja na injini ya treni yalitoka kwenye reli, huku mabehewa mawili yakipinduka kufuatia mlipuko huo mkubwa, treni hiyo ilikuwa ikisafirisha askari pamoja na familia zao waliokuwa wakirejea nyumbani kwa ajili ya sikukuu, ya Eid.
Serikali ya jimbo la Balochistan imesema kundi la waasi la Balochistan Liberation Army, ndilo lililohusika na shambulizi hilo likidaiwa kutekelezwa kwa njia ya kujitoa mhanga, kundi hilo lilidai kuhusika na tukio hilo muda mfupi baada ya mlipuko, kutokea.
Picha kutoka eneo la tukio zinaonesha mabehewa ya treni yaliyoteketea kwa moto, magari yaliyoharibika vibaya p...
- Title
- Polisi wawashikilia Wachina wanne kwa utekaji
- Runtime
- 7:47
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- Alichokisema Kihenzile mbele ya Waziri Mkuu
- Runtime
- 9:04
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU,KIKAO CHA THELATHINI NA SITA MEI 25, 2026
- Runtime
- 5:13:34
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU,KIKAO CHA THELATHINI NA SITA MEI 25, 2026
- Title
- VITA UKRAINE YACHUKUA SURA MPYA, RUSSIA YATUMIA KOMBORA LA KASI KUBWA
- Runtime
- 3:12
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Russia imefanya mashambulizi makubwa dhidi ya Ukraine usiku, kwa kutumia ndege zisizo na rubani (drones) pamoja na makombora kadhaa, hali iliyosababisha vifo vya watu wanne na kujeruhiwa kwa zaidi ya watu 100, katika maeneo mbalimbali nchini humo, huku Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema mji mkuu Kyiv ulikuwa shabaha kuu, ya mashambulizi hayo.
Milipuko mikubwa ilisikika usiku kucha katika jiji la Kyiv, huku majengo mengi ya makazi, shule, ukumbi wa opera na makumbusho yakiharibiwa vibaya, miongoni mwa maeneo yaliyoathirika ni Makumbusho ya Chornobyl ambayo maaofisa wa Ukraine wamesema, yameharibiwa kwa kiwango kikubwa baada ya kushambuliwa.
Wizara ya Ulinzi wa Russia imedai kutumia kombora la kisasa la kasi kubwa, aina ya Oreshnik katika mashambulizi hayo, ikisema hatua hiyo ilikuwa ni jibu kwa kile ilichodai kuwa, mashambulizi ya Ukraine dhidi ya miundombinu ya kiraia ya Russia, hata hivyo jeshi la Ukraine limekanusha kuwahi kulenga raia.
- Title
- LISSU AFIKISHWA MAHAKAMA KUU, KESI YA MGAWANYO WA MALI.
- Runtime
- 0:56
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Mwenyekiti wa Chama Cha Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Tundu Lissu, amefikishwa katika Mahakama kuu Masjala Ndogo ya Dar es salaam, Leo jumatatu Mei 25, 2026 kwa ajili ya kusikiliza maombi yake ya kuunganishwa katika kesi inayohusu mali za chama hicho.
Kesi hiyo itasikilizwa mbele ya Jaji Ngunyale ambapo Lissu atahudhuria akiwa katika nafasi yake ya uongozi ndani ya chama
Usikilizwaji wa kesi hiyo unatarajiwa kuanza saa 2:45 asubuhi huku .
- Title
- ALLAN OKELLO AFUNGUKIA BATO LAKE NA CHAMA, AMTAJA MESSI
- Runtime
- 10:30
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kule Simba kuna moto unaowashwa na kiungo wao Clatous Chama ambao mashabiki wa timu zingine hawaufurahii lakini Yanga nako kuna mtu mwingine ana balaa, huyu ni Allan Okello, vilevile wengine wanachukia kiwango chake. Sasa raia huyo wa Uganda ameamua kufunguka kuhusu Chama.
Chama tangu amerejea Simba kuanzia dirisha dogo la Januari 2026, namba zake zimeanza kushtua akifunga jumla ya mabao manane kati ya hayo, sita ameyafunga akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi wakati mawili aliyafunga alipokuwa Singida Black Stars.
Kiungo huyo pia amefanikiwa kutengeneza asisti sita ambazo zote amezipika akiwa hapo Simba na kumfanya kuhusika kwenye jumla ya mabao 14, lakini moto wake zaidi ni kwamba amebeba tuzo tano za mchezaji bora wa mechi katika michezo mitano mfululizo.
Okello naye ana balaa lake, akianzia dirisha dogo la Januari 2026 kama ilivyo kwa Chama, akifanikiwa kufunga mabao tisa akimfikia Prince Dube anayecheza naye pale Yanga ambaye yeye ameanza mwanzo ...
- Title
- DK MWIGULU: DINI HAZISIMAMISHI VIONGOZI NCHINI
- Runtime
- 3:42
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba amesema vyama vya siasa vilivyosajiliwa kikatiba ndivyo vyenye dhamana ya kisheria ya kupendekeza na kusimamisha wagombea katika nyadhifa mbalimbali za kuwakilisha wananchi, na siyo madhehebu ya dini.
Dk Mwigulu ameyasema hayo leo Jumamosi, Mei 23, 2026 wakati akihutubia mkutano wa hadhara na wananchi wa Mkoa wa Iringa.
Amesema mfumo wa uongozi nchini unazingatia Katiba kupitia vyama vya siasa pekee, vinavyotekeleza taratibu za kupata viongozi wa nchi kwa mujibu wa sheria.
“Nchi yetu hii, utaratibu wa kupata viongozi wakuu wa nchi ni kupitia vyama vya siasa. Hatujawahi kusimamisha wagombea wa madhehebu, tunatumia vyama vya siasa ndivyo Katiba inavyosema,” amesema Dk Mwigulu.
Aidha, ameonya vibaraka wenye nia ovu ya kuhatarisha na kuharibu amani nchini kwa kueneza habari potofu na zinazopotosha wananchi, akisisitiza kuwa hawatofanikiwa katika malengo yao.
- Title
- NI HUZUNI MWILI WA MCHINA ALIYEUAWA KIKATILI UKIAGWA MABIBO
- Runtime
- 3:06
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- MATUKIO YA UTEKAJI YAMUIBUA WAZIRI MKUU, ATOA MAAGIZO HAYA
- Runtime
- 4:56
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- DCEA YATEKETEZA KILO 504 ZA HEROINI MTWARA
- Runtime
- 3:58
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, imeteketeza kilo 504.36 za heroini zilizokamatwa kutoka kwa raia saba wa Iran katika Bahari ya Hindi ndani ya eneo tengefu la kiuchumi wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi.
Uteketezaji huo umefanyika leo Mei 23, 2026 kufuatia amri ya Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara iliyotaka vielelezo hivyo vilivyokamatwa kati ya Aprili 22 na 24, 2021 viharibiwe rasmi.
Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kupambana na biashara ya dawa za kulevya inayotishia usalama wa Taifa na afya ya jamii.
Amesema awali mamlaka hiyo pia iliteketeza kilo 355 za methamphetamine kutokana na dawa hizo kuwa katika mfumo unaoyeyuka haraka zinapopata joto.
- Title
- MWAMNYETO ATOA KAULI ILE ISHU YA KUJIFUNGA DHIDI YA DODOMA JIJI, YANGA IKIFA BAO 3-2
- Runtime
- 4:32
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Beki wa Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto, amesema kila mchezaji huweza kufanya makosa uwanjani, lakini athari na namna ya kupokewa kwake hutofautiana kulingana na mazingira.
Ameeleza makosa aliyoyafanya katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji iliyopigwa Mei 13, 2026, ambapo Yanga ilipoteza kwa mabao 3-2, tayari ameyaweka nyuma na hana muda wa kuyawaza tena.
Kwa sasa, anajielekeza kikamilifu katika mechi sita zijazo za Ligi Kuu Bara, akilenga kusaidia Yanga kupambana na kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Hadi sasa Yanga inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 57 ikifuatiwa na Simba katika nafasi ya pili na pointi 55.
...
- Title
- 'DRESS CODE' YA ALI KAMWE LEO NI SH7 MILIONI, AFUNGUKIA MECHI ZA SIMBA, MAPENZI
- Runtime
- 7:54
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
#samiasuluhuhassan #simbasc #yangasc #mashabiki #nbcpremeireleague #cafchampionsleague #cafconfiderationcup #ikulumawasiliano #entertainment #music #news #yangasc #simbasc #cafchampionsleague #mayele #highlights #cafconfiderationcup #riversunited #mashabiki #yangaleo #yanga #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko #entertainment #music #news #magoliyasimba #magoliyayanga #magoliyote #magoliyamayele #mayele #aziziki #manara #manaraleo #ikulumawasiliano...
- Title
- #live: BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU, KIKAO CHA 35 | MEI 22, 2026
- Runtime
- 3:48:36
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- KOCHA KANU AFAFANUA SABABU ZA KUMTOA KIPA METACHA
- Runtime
- 3:33
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- KOCHA MOALIN: HAIKUWA RAISI KUIFUNGA SINGIDA
- Runtime
- 3:09
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- ALI KAMWE: KILA MTU ASHINDE ZAKE
- Runtime
- 6:38
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- SALIBOKO MKALI WA BUTTERFLY ALIYEANZIA BAHARINI: BABA MZAZI AFUNGUKA
- Runtime
- 24:01
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- #live: BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA TATU, KIKAO CHA 33 | MEI 21, 2026
- Runtime
- 3:57:28
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
- Title
- MAAJABU YA CHAMA YAIBEBA SIMBA YAWAPONZA WENYEJI, YANGA vs SINGIDA PRESHA YAPANDA UCHAMBUZI WA NKINI
- Runtime
- 10:44
- Date posted
- 2 months ago
- Description
- Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
#samiasuluhuhassan #simbasc #yangasc #mashabiki #nbcpremeireleague #cafchampionsleague #cafconfiderationcup #ikulumawasiliano #entertainment #music #news #yangasc #simbasc #cafchampionsleague #mayele #highlights #cafconfiderationcup #riversunited #mashabiki #yangaleo #yanga #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko #entertainment #music #news #magoliyasimba #magoliyayanga #magoliyote #magoliyamayele #mayele #aziziki #manara #manaraleo #ikulumawasiliano...

