Azam TV
Goli la ubingwa | Madenge FC 1-0 Azimio FC | Imbeju Ndondo Cup 17/09/2026
- Title
- Goli la ubingwa | Madenge FC 1-0 Azimio FC | Imbeju Ndondo Cup 17/09/2026
- Runtime
- 1:20
- Date posted
- 30 days ago
- Description
- Azam TV
- Title
- MSHIKEMSHIKE - AZAM TV 18/09/2026
- Runtime
- 45:33
- Date posted
- 30 days ago
- Description
- Azam TV
- Title
- Goli la Kangwanda | Yanga SC 1-0 St. George | International Friendly 18/09/2026
- Runtime
- 1:13
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Yanga SC imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya St. George ya Ethiopia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa KMC Complex, Dar es Salaam.
Goli pekee la mchezo huu limefungwa na Albert Kangwanda dakika ya 60.
Hili ni goli...
- Title
- VIWANJANI | Mapumziko ya FIFA, fursa kwa Klabu kujiimarisha na kurekebisha mapungufu ya vikosi.
- Runtime
- 59:15
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Wachambuzi wa soka, Michael Hyera, Godlisten Muro na Frank Domayo wazungumza faida ya mapumziko ya FIFA kwa klabu katika kuimarisha vikosi vyao.
Domayo akitoa uzoefu wake amesema baadhi ya wachezaji hujiunga na timu za taifa, huku wengine wakibaki kwenye klabu zao na kucheza mechi za kirafiki wakati wa mapumziko hayo.
Amesema mechi hizo za kirafiki huwapa nafasi wachezaji ambao hawapati muda wa kutosha kucheza katika mechi za Ligi, hivyo kuwasaidia kuendelea kuwa katika ushindani na kujiandaa kwa mechi zinazofuata.
Azam TV
- Title
- Madenge FC Mabingwa Imbeju Ndondo Cup 2026
- Runtime
- 3:01
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Mabingwa Madenge FC wamekabidhiwa kombe lao baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azimio.
Azam TV
- Title
- MAHOJIANO MAALUM | 18/09/2026 | Fasila Adhiambo mchezaji wa Simba Queens.
- Runtime
- 24:25
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Mchezaji wa soka, Fasila Adhiambo amefunguka kuhusu historia ya maisha yake ndani ya mchezo huo, akieleza safari yake kutoka hatua za mwanzo kabisa hadi kufikia kuwa miongoni mwa wachezaji wa kulipwa katika soka la wanawake.
Akizungumza kuhusu mafanikio yake, Fasila amesema safari hiyo haikuwa rahisi kutokana na changamoto mbalimbali alizokutana nazo, lakini kupitia nidhamu, kujituma na mchango wa wazazi katika kuendeleza kipaji chake ameweza kufikia hatua aliyonayo leo.
Mahojiano haya yamefanywa na Sports Lady, Timzo Kalugira.
Azam TV
- Title
- Magoli | Burundi 2-0 Kenya | U20 AFCON CECAFA Qualifiers 17/09/2026
- Runtime
- 2:31
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #CECAFAU20Championship Chuma zote mbili zilizowekwa kambani na Nshirimana.
FT: Burundi 2-0 Kenya
Real Betis vs Getafe iko LIVE #ZBC2
#U20AFCONCECAFAQualifiers #CECAFAU20 #U20AFCONQualifiers #Burundi #Kenya #BurundiKenya
- Title
- Azam FC 0-2 Simba SC | Magoli kwa lugha ya Kiingereza | NBC PL 16/09/2026
- Runtime
- 3:48
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Sikiliza magoli yote mawili yalivyotangazwa kwa lugha ya Kiingereza na Peter Otai.
Ilikuwa ni Mzizima Derby ya Ligi Kuu ay NBC, mchezo ukipigwa Azam Complex, Chamazi... Magoli yakifungwa na Nathan Idumba goli la kujifunga na Clatous Chama.
- Title
- Magoli | Djibouti 0-3 Sudan | U20 AFCON CECAFA Qualifiers 17/09/2026
- Runtime
- 3:53
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #CECAFAU20Championship Vyuma vitatu vya nguvu, Sudan wakitoa darasa…
FT: Djibouti 0-3 Sudan
Wafungaji ni Wail Galal Omer aliyefunga mawili, na Ibrahim Samani.
- Title
- MZIZIMA DERBY | Gharib Mzinga alivyoyafungua matangazo ya mechi ya Azam FC dhidi ya Simba SC
- Runtime
- 1:58
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #MzizimaDerby: Mtangazaji wa soka @gharib_mzinga23 alianza kwa kukupeleka Kariakoo ambako ndio maskani ya Simba SC, kisha akakupeleka Mzizima ambako ndio Makao Makuu ya Azam FC alafu akakurudisha Chamazi ambako ‘mbungi’ ilipigwa.
Ni kwenye ufunguzi wa mechi ya jana Septemba 16 ya #MzizimaDerby kati ya Azam FC dhidi ya Simba SC.
FT: Azam FC 0-2 Simba SC
#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi #AzamFC #SimbaSC #AzamSimba
- Title
- Historia yaandikwa MzizimaDabi! Simba SC yachukua alama zote tatu.
- Runtime
- 45:56
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Wachambuzi wa soka Ramadhani Mbwaduke, Michael Hyera na Khalid Chukuchuku watia neno ushindi wa Mnyama mbele ya Matajiri wa Jiji.
Mbwaduke amesema iwapo Simba SC itaendelea kutumia nafasi inazozitengeneza kwa ufanisi na kujitendea haki katika umaliziaji, timu hiyo inaweza kuonesha kiwango bora zaidi katika michezo inayofuata.
Huku Chukuchuku anasema Mzizima Dabi ni miongoni mwa michezo inayotuonesha ufundi, mbinu na umakini kutokana na ushindani unaoambatana na mechi hizo japo katika mchezo wa jana ladha hiyo haikuwepo kwa asilimia zote.
Azam TV
- Title
- Azam 0-2 Simba | Furaha ya mashabiki | Chilambo, Ibwe watoa neno baada ya mechi | NBC PL 16/09/2026
- Runtime
- 20:12
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Azam TV
- Title
- Azam FC 0-2 Simba SC | Highlights | Mzizima Derby | NBC PL 16/09/2026
- Runtime
- 13:51
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- MZIZIMA DERBY | Magoli mawili, moja likiwa ni la kujifunga kupitia kwa Nathan Fasika Idumba na Clatous Chama yameipa Simba SC ushindi wa 2-0 dhidi ya Azam FC, katika #MzizimaDerby ya Ligi Kuu ya NBC iliyopigwa kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi.
- Title
- Magoli | Azam FC 0-2 Simba SC | Mzizima Derby | NBC PL 16/09/2026
- Runtime
- 3:23
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- MZIZIMA DERBY | Magoli mawili, moja likiwa ni la kujifunga kupitia kwa Nathan Fasika Idumba na Clatous Chama yameipa Simba SC ushindi wa 2-0 dhidi ya Azam FC, katika #MzizimaDerby ya Ligi Kuu ya NBC iliyopigwa kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi.
- Title
- Yanga SC 1-0 Geita Gold FC | Walichozungumza makocha baada ya mechi
- Runtime
- 5:18
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #NBCPL “… Mungu alikuwa upande wao”
Kocha wa Geita Gold FC, Zuberi Katwila anaeleza kiufundi kilichotokea, anasema waliuliza maswali lakini mipira iligoma kuingia nyavuni, anasema wamefungwa goli jepesi…
Kwa upande wake Kocha wa Yanga anaanza kwa kuhoji kadi nyekundu aliyopata Aziz Ki, anawapongeza wachezaji wake kwa kupambana na kushinda licha ya kuwa pungufu dimbani akisema “…tumeonesha kwamba ni timu ya kibingwa”.
Nyota wa mchezo ni Maxi Nzengeli ana anazungumza machache akiipeleka tuzo yake ‘kwa Mungu’.
FT: Yanga SC 1-0 Geita Gold FC
- Title
- MZIZIMA DERBY | Vimbwanga, vituko, tambo za mashabiki wa AzamFC, Simba SC kutoka Mabibo Sokoni
- Runtime
- 20:57
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- MZIZIMA DERBY: “Nyumba naweka bondi kwasababu Azam imfunge Simba”
Ni tambo za Chinkonk, shabiki wa Azam FC, kutoka Mabibo Sokoni Dar es Salaam.
Shabiki huyo anasema yupo tayari kulala nje kama tenga lakini nyumba anaiweka bondi akiamini Azam FC itaibuka na ushindi leo kwenye #MzizimaDerby.
Ni tambo kuelekea #MzizimaDerby ambayo itapigwa Azam Complex, Chamazi saa1:00 usiku LIVE #AzamSports1HD
- Title
- MZIZIMA DERBY | Shabiki Simba asema Libasse Gueye anapata namba Manchester United
- Runtime
- 1:07
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- VIWANJANI: “Libasse Gueye anaanza Manchester United”
Hizo ni tambo za shabiki wa Simba SC, kutoka Mabibo Sokoni Dar es Salaam ambaye anasema nyota wao, Libasse Gueye anaweza kumweka benchi Marcus Rashford kutokana na ubora wake anaouonesha pale Msimbazi.
Shabiki huyo anayeitwa Madega Junior anasema Libasse ni Messi wa Senegal.
Ni tambo kuelekea #MzizimaDerby ambayo itapigwa Azam Complex, Chamazi saa1:00 usiku LIVE #AzamSports1HD
#MzizimaDerby #AzamFC #SimbaSC #Viwanjani
- Title
- Simba SC 6-1 Mighty Wonderers | Neno la makocha baada ya mechi | CAF CL 13/09/2026
- Runtime
- 3:36
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Kocha wa Simba, Steve Barker ameeleza furaha yake baada ya ushindi, amewapongeza wachezaji kwa kazi waliyofanya, amezungumzia kiwango cha Libase Gueye, amejipongeza mwenyewe kwa 'sub' alizofanya kuzaa matunda.
Kwa upande wa Mighty Wonderers, kocha wake ameeleza kushangazwa na kiwango walichokionesga leo akisema "siyo kiwango chetu".
Pia ameukubali muziki wa Simba ya leo akisema leo wamecheza vizuri kuliko mchezo uliopita.
FT: Simba SC 6-1 Mighty Wanderers (Agg: 7-1)
- Title
- Magoli | Uganda 4-1 Djibouti | U20 AFCON CECAFA Qualifiers 15/09/2026
- Runtime
- 3:55
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Vijana wa Uganda U20 wamewanyoosha Djibouti kwa kichapo cha mabao 4-2 katika mchezo wa kwanza kabisa wa michuano ya kufuzu AFCON U20 kutoka ukanda wa CECAFA.
Michuano hii inapigwa kwenye Dimba la Uhuru, Dar es Salaam...
- Title
- Magoli | South Sudan 0-4 Burundi | U20 AFCON CECAFA Qualifiers 15/09/2026
- Runtime
- 4:13
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Hivi ndivyo vijana wa Burundj U20 walivyowashushia kichapo cha 4-0 wenzao wa Sudan Kusini.
Ni katika michuano ya kufuzu AFCON U20 kutoka ukanda wa CECAFA inayofanyika kwenye Dimba la Uhuru, Dar es Salaam.
- Title
- Magoli | Tanzania 3-0 Rwanda | U20 AFCON CECAFA Qualifiers 15/09/2026
- Runtime
- 2:38
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #CECAFAU20Championship Magoli yote matatu ya Ngorongoro Heroes…. Wafungaji ni Faraji Kayanda, Juma Abushiri ‘Chuga Boy’ na Evastus Lukanimi
FT: Tanzania 3-0 Rwanda.
Hii ni michuano ya kufuzu AFCON U20 kutoka ukanda wa CECAFA...
#U20AFCONCECAFAQualifiers #CECAFAU20 #U20AFCONQualifiers #NgorongoroHeroes #TanzaniaRwanda
- Title
- Yanga SC 1-0 Geita Gold FC | NBC Premier League 15/09/2026
- Runtime
- 10:55
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Goli pekee kutoka kwa Farouk Oumar Komara limeipa Yanga alama tatu, ikishinda 1-0 dhidi a Geita Gold FC, mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa kwenye Dimba la KMC Complex, Dar es Salaam.
Hili hapa goli, Komara akimalizia kona ya Maxi Nzengeli.
- Title
- MSHIKEMSHIKE - AZAM TV 15/09/2026
- Runtime
- 28:04
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Azam TV
- Title
- Goli la Komara | Yanga SC 1-0 Geita Gold FC | NBC Premier League 15/09/2026
- Runtime
- 1:27
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Goli pekee kutoka kwa Farouk Oumar Komara limeipa Yanga alama tatu, ikishinda 1-0 dhidi a Geita Gold FC, mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa kwenye Dimba la KMC Complex, Dar es Salaam.
Hili hapa goli, Komara akimalizia kona ya Maxi Nzengeli.
- Title
- Kocha Francis Baraza wa Pamba Jiji ataja sababu za timu yake kupepesuka Ligi Kuu
- Runtime
- 9:25
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- VIWANJANI: “Ligi imekuwa ngumu hasa kwa upande wangu”
Kocha wa Pamba Jiji, Franchis Baraza anasema kwa sasa wanapitia kipindi kigumu huku akitaja miongoni mwa sababu kuwa ni majeraha yaliyowapata wachezaji saba siku chache baada ya kuanza maandalizi ya msimu mpya.
Baraza anasema sababu nyingine ni wachezaji watano wapya ambao walijiunga na timu wakati ligi imeshaanza.
Kocha huyo anasema kuondoka kwa baadhi ya wachezaji muhimu waliotumika kwenye msimu uliopita japo anaongeza kuwa wapo wachezaji ambao wamewasajili kwa ajili ya kuziba nafasi zao.
Ni mahojiano maalumu ya Kocha Francis Baraza yaliyofanywa kupitia kipindi cha #Viwanjani kwa njia ya mtandao.
#Viwanjani
- Title
- MZIZIMA DERBY | Kocha Simba asema wapo tayari kukabiliana na Azam FC
- Runtime
- 8:18
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- MZIZIMA DERBY: Kocha wa Simba SC, Steve Barker anasema moja ya sababu za wao kukosa taji la NBC Premier League msimu uliopita ni kupoteza alama nne mbele ya Azam FC na kuchukua alama mbili kwa Yanga SC.
Kocha huyo anasema kesho Septemba 16, 2026 wanakwenda kukutana na mechi ngumu lakini wao kama Simba mar azote wapo tayari kukabiliana na changamoto yoyote iliyopo mbele yao.
Kwa upande wake mchezaji Nathaniel Chilambo anasema wanajua wanakwenda kukabiliana na timu yenye wachezaji wazuri lakini wapo tayari kwa mchezo.
Mechi itapigwa saa 1:00 usiku na itakuwa LIVE #AzamSports1HD
#MzizimaDerby #AzamFC #SimbaSC
- Title
- MZIZIMA DERBY | Kocha Ibenge, Manula waizungumzia mechi yao dhidi ya Simba
- Runtime
- 11:23
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- MZIZIMA DERBY: “Kesho ni mechi kubwa”
Kocha wa Azam FC, Florent Ibenge anasema taswira inajieleza kwamba kesho Septemba 16, 2026 inakwenda kuchezwa mechi kubwa na wao wamejiandaa kwa mechi hiyo.
Kocha huyo anasema kwa aina ya uchezaji wa Simba, mechi hiyo inakwenda kuwa ngumu.
Kwa upande wake golikipa Aishi Manula anasema hawakuanza vizuri ligi lakini kadri wanavyozidi kucheza, ndivyo ambavyo wanatarajia kukusanya alama zaidi.
Mechi itapigwa saa 1:00 usiku na itakuwa LIVE #AzamSports1HD
#MzizimaDerby #AzamFC #SimbaSC
- Title
- MSHIKEMSHIKE - AZAM TV 14/09/2026
- Runtime
- 50:58
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Azam TV
- Title
- ZILIZOBAMBA MITANDAONI | Mashabiki wa Simba ni full shangwe, harusi ya Fatma Chikawe ni raha tupu
- Runtime
- 18:10
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- ZILIZOBAMBA MITANDAONI: Jamani huyu mtangazaji @ngodaalwatan huu mtindo wa ‘kunema’ dufu ameutoa wapi…..????
Hiki kibega ni kama kinataka kuanguka.
Ni #Zilizobamba mitandaoni
#Viwanjani #Zilizobamba
- Title
- Kocha Katwila wa Geita Gold anasema amejiandaa kucheza na Yanga isiyo na uchovu
- Runtime
- 3:05
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- YANGA vs GEITA GOLD: “Kiwango cha mpinzani ni kikubwa”
Kocha Zuberi Katwila wa Geita Gold, anasema wanafahamu ukubwa wa mpinzani wao na wamejipanga kucheza kitimu zaidi ili kukabiliana na Yanga.
Katwila anasema amejiandaa kucheza na Yanga ambayo anaamini haina uchovu hata kama imetoka kucheza mechi ya kimataifa.
Mechi ni kesho Septemba 15, 2026 saa 1:00 usiku LIVE #AzamSports1HD
#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates
- Title
- Kocha Manqoba wa Yanga amtaja Libasse Gueye wa Simba wakati akiizungumzia Geita Gold
- Runtime
- 4:39
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- YANGA vs GEITA GOLD: Kocha wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi amesifu uwezo wa Kocha Zuberi Katwila wa Geita Gold huku akiongeza kuwa mwalimu huyo huwa habadili sana kikosi chake japo hubadili muuondo wa uchezaji.
Kocha Manqoba amezungumzia namna Kocha Katwila alivyowapanga wachezaji wake kwenye mechi dhidi ya Simba huku akimtaja Libasse Gueye.
Kocha huyo anasema wachezaji wake wanatengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini hazitumiki ipasavyo na hapo wanapaswa kufanyia kazi.
Kwa upande wake beki Mohamed Hussein Zimbwe, anasema wameitazama Geita Gold wameangalia mazuri yao na mapungufu yao watayafanyia kazi.
Mechi ni kesho Septemba 15, 2026 saa 1:00 usiku LIVE #AzamSports1HD
#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates
- Title
- Magoli | KVZ FC 0-3 Al Swehly | CAF Champions League 13/09/2026
- Runtime
- 2:27
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #CAFCL Magoli yote matatu waliyofungwa KVZ wakiwa nyumbani, kwenye mchezo wa marudiano, Ligi ya Mabingwa Afrika. Amaan Stadium, Zanzibar.
Kwa matokeo haya, KVZ wanatupwa nje kwa jumla ya magoli 4-0 baada ya kupoteza 1-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza ugenini.
FT: KVZ FC 0-3 Al Swehly (Agg: 0-4).
#CAFChampionsLeague #KVZFC #AlSwehlySC
- Title
- Magoli | Kagera Sugar 1-1 Fountain Gate FC | NBC PL 13/09/2026
- Runtime
- 2:19
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #NBCPL Magoli yote mawili, akitangulia Jesto Masanja kwa header, lakini akajifunga Andrew Vicent Chikupe.
FT: Kagera Sugar 1-1 Fountain Gate.
Hii ni Ligi Kuu ya NBC ..
#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #KageraSugar #FountainGate
- Title
- Singida BS 3-0 Al Ghazala Wau | Highlights | Kombe la Shirikisho Afrika - 13/09/2026
- Runtime
- 4:23
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- CAFCC: Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mechi ya Singida BS ikiifunga Al Ghazala, kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Jonathan Sowah akweka mbili huku Henry David akifunga goli moja.
Mechi imepigwa katika dimba la Azam Complex, Chamazi.
FT: Singida BS 3-0 Al Ghazala (Agg: 10-1)
#CAFCC #KombeLaShirikishoAfrika #CAFConfederationCup #SingidaBS #AlGhazala
- Title
- Simba SC 6-1 Mighty Wanderes | Highlights | Ligi ya Mabingwa Afrika - 13/09/2026
- Runtime
- 12:59
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #CAFCL: Tazama matukio yote muhimu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Mighty Wanderers.
Clatous Chama amefunga magoli mawili, Libasse Gueye amefunga mawili, Keletso Makgalwa amefunga moja na Morice Abrahamu akaweka moja.
Goli la Mighty Wanders limefungwa na Isac Kaliati.
FT: Simba SC 6-1 Mighty Wanderers (Agg: 7-1)
#CAFCL #LigiYaMabingwaAfrika #CAFChampionsLeague #SimbaSC #MightyWanderers
- Title
- Pamba Jiji FC 1-3 TRA United | Highlights | NBC Premier League 13/09/2026
- Runtime
- 4:19
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Pamba Jiji FC wamekula kichapo cha 3-1 nyumbani kwenye Dimba lao la CCM Kirumba, kutoka kwa wakusanya mapato, TRA United., katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
TRA wamepata mabao yao yote kipindi cha kwanza kupitia kwa Ani Elijah, Nonyem Okorocha na Emmanuel Okorocha huku Pamba wakipata bao lao kupitia kwa Abdulkarim Iddy.
Tazama highlights
- Title
- SIMBA SC 6-1 Mighty Wanderers | Ulumbi wa Mpenja kabla ya mechi ya Simba
- Runtime
- 2:30
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #CAFCL: Msikie Sauti ya Radi @baraka_mpenja alivyoyafungua matangazo ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kati ya Simba dhidi ya Maighty Wanderers.
Mpenja ameanzia bandarini, akaenda TAZARA, akarudi Posta, kisha stesheni ya SGR ya Magufuli Dar es Salaam na maeneo mengine. Lakini kuna kitu kakigusia kuhusu dimba la Uhuru. Je, ulikuwa wajua…???
FT: Simba SC 6-1 Mighty Wanderers (Agg: 7-1)
Ilikuwa LIVE #AzamSports2HD
#CAFCL #LigiYaMabingwaAfrika #CAFChampionsLeague #SimbaSC #MightyWanderers
- Title
- Singida BS 3-0 Al Ghazala Wau | Magoli | Kombe la Shirikisho Afrika - 13/09/2026
- Runtime
- 3:19
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- CAFCC: Tazama chum zote tatu za Singida BS ikiifunga Al Ghazala, kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Jonathan Sowah akweka mbili huku Henry David akifunga goli moja.
Mechi imepigwa katika dimba la Azam Complex, Chamazi.
FT: Singida BS 3-0 Al Ghazala (Agg: 10-1)
Ilikuwa LIVE #AzamSports5HD
#CAFCC #KombeLaShirikishoAfrika #CAFConfederationCup #SingidaBS #AlGhazala
- Title
- Pamba Jiji 1-3 TRA United | Magoli | NBC Premier League - 13/09/2026
- Runtime
- 5:27
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- NBCPL: Tazama magoli yote manne yaliyofungwa kwenye mchezo wa NBC Premier League kati ya Pamba Jiji dhidi ya TRA United.
Magoli ya TRA United yamefungwa na Emanuel Mwanengo, Nonyem Okorocha ambaye amejifunga na Anni Elija.
Goli la Pamba Jiji limefungwa na Abdulkarim Yunusi.
Mechi imepigwa katika dimba la CCM Kirumba, Mwanza
FT: Pamba Jiji 1-3 TRA United
#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #PambaJiji #TRAUnited
- Title
- Simba SC 6-1 Mighty Wanderes | Magoli | Ligi ya Mabingwa Afrika - 13/09/2026
- Runtime
- 9:47
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #CAFCL: Tazama magoli yote saba yaliyofungwa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Mighty Wanderers.
Clatous Chama amefunga magoli mawili, Libasse Gueye amefunga mawili, Keletso Makgalwa amefunga moja na Morice Abrahamu akaweka moja.
Goli la Mighty Wanders limefungwa na Isac Kaliati.
FT: Simba SC 6-1 Mighty Wanderers (Agg: 7-1)
#CAFCL #LigiYaMabingwaAfrika #CAFChampionsLeague #SimbaSC #MightyWanderers
- Title
- Polisi Tanzania 2-0 Mbeya City | Highlights | NBC Premier League - 12/09/2026
- Runtime
- 7:30
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #NBCPL: Chuma mbili za Anuary Jabir wakati Polisi Tanzania ikiichapa Mbeya City ndani ya dimba la Sheikh Amri Abeid.
FT: Polisi Tanzania 2-0 Mbeya City
#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #PolisiTanzania #MbeyaCity #PLS #MCC
- Title
- Coastal Union 2-1 JKT Tanzania | Magoli | NBC Premier League - 12/09/2026
- Runtime
- 4:55
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #NBCPL: Tazama magoli yote matatu yaliyofungwa kwenye mchezo kati ya Coastal Union dhidi ya JKT Tanzania.
Magoli ya CoASTAL Union yamefungwa na Maabad Maulid na Shiza Kichuya, huku goli la JKT Tanzania likifungwa na Mohamed Otali
FT: Coastal Union 2-1 JKT Tanzania
#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #CoastalUnion #JKTTanzania
- Title
- Magoli Yanga SC 2-1 Gaborone United | Highlights | Ligi ya Mabingwa Afrika - 12/09/2026
- Runtime
- 9:09
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #CAFCL | Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga SC dhidi ya Gaborone United.
Magoli ya Yanga yamefungwa na Peter Shalulile na Cheikh Toure.
Goli la Gaborone United limewekwa nyavuni na Lebogano Ditsele.
Mechi imepigwa katika dimba la Azam Complex, Chamazi.
FT: Yanga SC 2-1 Gaborone United (Agg: 3-2)
#CAFCL #CAFChampionsLeague #LigiYaMabingwaAfrika #SeleDay #YangaSC #GaboroneUnited #YangaGaborone
- Title
- Yanga 2-1 Gaborone United | Shalulile asisitiza kumuomba Mungu
- Runtime
- 2:23
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #CAFCL | “Haikuwa mechi nyepesi”
Mfungaji wa goli la kwanza la Yanga SC, Peter Shalulile anasema kwa kumuomba Mungu, itasaidia timu kuwa bora zaidi kuliko mwaka uliopita na hilo linawezekana.
Lebogano Ditsele wa Gaborone United anasema mpango wao hakuwa kuruhusu goli mapema, lakini walipofungwa mambo yalibadilika.
FT: Yanga SC 2-1 Gaborone United (Agg: 3-2)
#CAFCL #CAFChampionsLeague #LigiYaMabingwaAfrika #SeleDay #YangaSC #GaboroneUnited #YangaGaborone
- Title
- Yanga 2-1 Gaborone United | Kocha Yanga asema wangeshinda hata magoli saba
- Runtime
- 4:05
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #CAFCL | “Tungeimaliza mechi na magoli zaidi ya saba”
Kocha wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi anasema kama wachezaji wake wangetumia vema nafasi walizotengeneza, basi wangeshinda magoli zaidi ya saba.
Kocha wa Gaborone United anasema Yanga ilikuwa bora dakika 15 za kipindi cha kwanza, lakini kipindi cha pili walikishika wao.
FT: Yanga SC 2-1 Gaborone United (Agg: 3-2)
#CAFCL #CAFChampionsLeague #LigiYaMabingwaAfrika #SeleDay #YangaSC #GaboroneUnited #YangaGaborone
- Title
- Magoli Yanga SC 2-1 Gaborone United | Magoli | Ligi ya Mabingwa Afrika - 12/09/2026
- Runtime
- 3:31
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #CAFCL | Tazama magoli yote matatu yaliyofungwa kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga SC dhidi ya Gaborone United.
Magoli ya Yanga yamefungwa na Peter Shalulile na Cheikh Toure.
Goli la Gaborone United limewekwa nyavuni na Lebogano Ditsele.
Mechi imepigwa katika dimba la Azam Complex, Chamazi.
FT: Yanga SC 2-1 Gaborone United (Agg: 3-2)
#CAFCL #CAFChampionsLeague #LigiYaMabingwaAfrika #SeleDay #YangaSC #GaboroneUnited #YangaGaborone
- Title
- Mashabiki wa Yanga waliweka bleach palepale Azam Complex, Chamazi
- Runtime
- 2:00
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #CAFCL | Tazama shughuli za kiuchumi zinazofanyika Chamazi na viunga vyake huku sauti ya mtangazaji wa soka @gharib_mzinga23 ikisimulia matukio mbalimbali kulekea mechi ya Yanga SC dhidi ya Gaborone United.
Kumbe ‘bleach’ ziliwekwa palepale Chamazi.
HT: Yanga SC 1-0 Gaborone United
LIVE #AzamSports2HD
#CAFCL #CAFChampionsLeague #LigiYaMabingwaAfrika #SeleDay #YangaSC #GaboroneUnited #YangaGaborone
- Title
- Polisi Tanzania 2-0 Mbeya City | Magoli | NBC Premier League - 12/09/2026
- Runtime
- 2:46
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- #NBCPL: Chuma mbili za Anuary Jabir wakati Polisi Tanzania ikiichapa Mbeya City ndani ya dimba la Sheikh Amri Abeid.
FT: Polisi Tanzania 2-0 Mbeya City
#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #PolisiTanzania #MbeyaCity #PLS #MCC
- Title
- WEDNESDAY NIGHT LIVE | Safari ya Mafanikio ya Basketball U16; Ismail Mbise na Sarif Hassan.
- Runtime
- 52:24
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Ni kocha mkuu wa U16 Taifa na mchezaji wa mpira wa Kikapu Sarif Hassan ndani ya kipindi cha #WednesdayNightLIVE ya Septemba 1, 2026 na #PatrickNyembera wakieleza kwa undani panda shuka ya mchezo huo mpaka kufikia mfanikio ambayo Taifa linajivunia.
Mbise pia amefunguka mikakati mizito ya kuung'arisha mpira wa Kikapu na kuuweka kwenye ramani ya soka la kimataifa.......
Wednesday Night Live ni kila Jumatano saa 1:00 usiku #AzamSports3HD
- Title
- KURASA ZA MWISHO | Tanzanite Queens Yaaga Kombe la Dunia Poland, Yanga na Simba Kibaruani CAFCL.
- Runtime
- 41:07
- Date posted
- 1 month ago
- Description
- Wahariri wa magazeti ya michezo ambao pia ni wachambuzi wa soka wajadili Majukumu ya kocha Bakari Shime kwa timu za wanawake, Yanga Vs Gaborone, Simba Vs Mighty Wanderers Ligi ya Mabingwa Afrika.
Azam TV

