Azam TV
NGAO YA JAMII 2026 | Tambo za Mashabiki wa 'Chuga' , Ni Yanga au Simba?
- Title
- NGAO YA JAMII 2026 | Tambo za Mashabiki wa 'Chuga' , Ni Yanga au Simba?
- Runtime
- 6:15
- Date posted
- 19 days ago
- Description
- AMSHAAMSHA NGAO YA JAMII | ‘‘tutawapiga kama ngoma’’, ni kauli na tambo za mashabiki wa Yanga na Simba jijini Arusha ikiwa ni kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii 2026 utakaowakutanisha miamba ya soka nchini.
Ni Yanga vs Simba, mechi itakayopigwa saa 2:30 usiku.
Iko LIVE kupitia #AzamSports1HD
Imeandaliwa na @rajjmsangi
#NgaoYaJamii2026 #KariakooDerby #YangaSimba
- Title
- VIWANJANI | Uchambuzi ubora wa Steve Barker na Manqoba Mngqith kuelekea Ngao ya Jamii.
- Runtime
- 58:05
- Date posted
- 19 days ago
- Description
- Fortunatus Kasomfi, mtanzania anayeishi Afrika Kusini amezungumzia ubora na falsafa za makocha wawili kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii, akimtaja Steve Barker kuwa na uwezo mkubwa katika kulijenga na kuliongoza eneo la kiungo, huku Manqoba Mngqithi akimuelezea kuwa imara zaidi katika eneo la ushambuliaji.
Azam TV
- Title
- VIWANJANI | Mjadala Dabi ya Ngao ya Jamii.
- Runtime
- 47:30
- Date posted
- 19 days ago
- Description
- Ramadhani Mbwaduke amesema anatarajia mchezo wa Ngao ya Jamii utakaowakutanisha watani wa jadi Yanga SC dhidi ya Simba SC kuwa wa Ushindani na wa kiufundi kutokana na falsafa za makocha wa klabu hizo.
Azam TV
- Title
- KARIAKOO DERBY | Vita ya maneno ya mashabiki Yanga, Simba
- Runtime
- 3:09
- Date posted
- 19 days ago
- Description
- #KariakooDeby: Tazama vita ya maneno kati Dkt. Mohamed ambaye ni shabiki wa Simba SC na God Yanga ambaye ni shabiki wa Yanga SC.
Wawili hao wamekutana kwenye boti ya Kilimanjaro IX wakielekea Zanzibar kwa ajili ya #KariakooDerby
Mechi ni saa 2:30 usiku LIVE #AzamSports1HD
#Viwanjani #KariakooDerby #YangaSC #SimbaSC
- Title
- VIWANJANI | Mjadala Kariakoo Dabi kutimua vumbi kesho Agosti 12 Coastal Union Festival kufana leo.
- Runtime
- 1:06:45
- Date posted
- 19 days ago
- Description
- Mchambuzi wa soka Frank Domayo amesema mchezo huo unatarajiwa kuwa wa kiufundi; huku ukiwa jukwaa la kwanza la kupima ubora wa wachezaji wapya waliosajiliwa kwa timu zote mbili baada za zile mechi za kirafiki.
Hyera anaamini nyota waliokuwepo kwenye vikosi vya msimu uliopita wanaweza kupata nafasi zaidi katika mchezo huo kutokana na uzoefu na viwango walivyoonesha msimu uliopita.
Afisa Habari wa Coastal Union, Hussein Mchomvu amesema maandalizi ya tamasha la klabu hiyo yamekamilika kwa asilimia 100.
Mchomvu amewahimiza mashabiki wa Coastal Union kujitokeza kwa wingi kushuhudia tamasha hilo, akieleza kuwa kuna mambo mbalimbali ya kuvutia, ikiwemo 'surprise' kedekede walizoandaliwa.
Azam TV
- Title
- COASTAL UNION FESTIVAL 2026 | Hii ndiyo suprise ya Coastal Union
- Runtime
- 8:54
- Date posted
- 20 days ago
- Description
- COASTAL UNION FESTIVAL 2026 | Supraizi ya Coastal Union ndani ya tamasha leo ni hii hapa...
Msikilize Afisa Habari, Hussein Mchomvu anavyoisherehesha.
IKO LIVE kupitia #AzamSports1HD
Mhariri | @rajjmsangi
#CoastalUnion #Azamtvsports
- Title
- Wachezaji waliotambulishwa na Coastal Union hawa hapa
- Runtime
- 11:09
- Date posted
- 20 days ago
- Description
- Azam TV
- Title
- Afisa Habari wa Coastal Union ameingi kwa namna hii...
- Runtime
- 2:52
- Date posted
- 20 days ago
- Description
- COASTAL UNION FESTIVAL 2026 | Tazama namna ambavyo Afisa Habari wa Coastal Union, Hussein Mchomvu alivyotinga ndani ya dimba....!amesindikizwa na burudani hii.
Shughuli hii inafanyika katika dimba la CCM Mkwakwani, Tanga.
IKO LIVE kupitia #AzamSports1HD
Mhariri | @rajjmsangi
#CoastalUnion #Azamtvsports
- Title
- COASTAL UNION FESTIVAL 2026 | Alichokisema Rais wa TFF, Wallace Karia uwanja wa Mkwakwani
- Runtime
- 1:40
- Date posted
- 20 days ago
- Description
- COASTAL UNION FESTIVAL 2026 | ''leo tunajaza uwanja ila tunapocheza watu hawaji'', Rais wa Shirikisho la Mpira Nchini (TFF), Wallace Karia akiwasisitiza viongozi wa Mkoa wa Tanga kuwa na utamaduni wa kuongeza hamasa kwa mashabiki.
Shughuli hii inafanyika katika dimba la CCM Mkwakwani, Tanga.
IKO LIVE kupitia #AzamSports1HD
Mhariri | @rajjmsangi
#CoastalUnion #Azamtvsports
- Title
- COASTAL UNION FESTIVAL 2026 | Waziri Aweso alivyokabidhiwa jezi mpya ya msimu
- Runtime
- 4:10
- Date posted
- 20 days ago
- Description
- COASTAL UNION FESTIVAL 2026 | Tazama namna ambavyo Mgeni Rasmi, Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani, Jumaa Aweso alivyokabidhiwa jezi na uongozi wa Coastal Union.
Shughuli hii inafanyika katika dimba la CCM Mkwakwani, Tanga.
IKO LIVE kupitia #AzamSports1HD
Mhariri | @rajjmsangi
#CoastalUnion #Azamtvsports
- Title
- Selemani Mwalimu ndani ya Yanga SC , Licha ya kutambulishwa Simba Day.
- Runtime
- 21:56
- Date posted
- 20 days ago
- Description
- Mchambuzi wa soka Frank Domayo amesema uamuzi wa mchezaji kujiunga na klabu nyingine mara nyingi hutokana na matakwa yake binafsi akizingatia maslahi yake ya kitaaluma na kifedha.
Domayo amesisitiza kuwa katika soka la kisasa mchezaji hufanya maamuzi kulingana na kile anachoona kitamnufaisha zaidi katika maisha na kazi yake.
Azam TV
- Title
- NGAO YA JAMII 2026: Kocha Barker aweka wazi walivyojipanga kuwavaa Yanga SC
- Runtime
- 1:07
- Date posted
- 20 days ago
- Description
- NGAO YA JAMII 2026 | Kocha wa Simba SC, Steve Barker amesema wamejiandaa vizuri kwa dabi dhidi ya Yanga kesho Agosti 12, 2026 wakilenga kuanza msimu wa 2026/27 kwa kutwaa Ngao ya Jamii.
Barker amesema wanafahamu ubora wa Yanga, hivyo maandalizi yamejikita katika maeneo ya kiufundi, kimwili na kisaikolojia ili kuwa tayari kwa ushindani wa mchezo huo.
Kwa upande wake mchezaji wa timu hiyo, Nickson Kibabage amesema mchezo wa kesho ni mgumu na muhimu kwa kikosi chao hivyo aliyejiandaa vizuri ataibuka mshindi.
Ni maandalizi kuelekea game ya Ngao ya Jamii , Yanga vs Simba Agosti 12 LIVE #AzamSports1HD
#NgaoYaJamii2026 #KariakooDerby #YangaSimba
- Title
- NGAO YA JAMII 2026: Kocha Manqoba aeleza kikosi chake kilivyojipanga kwa Simba SC
- Runtime
- 1:15
- Date posted
- 20 days ago
- Description
- NGAO YA JAMII 2026 | Kocha wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi amesema ana imani na kikosi chake na anaamini kina uwezo wa kucheza soka safi licha ya kuwa na muda mfupi wa kukiunganisha.
Mngqithi amesema katika mchezo wa Ngao ya Jamii wa kesho matokeo pekee siyo jambo la msingi bali pia kuhakikisha mashabiki wanafurahia aina ya soka watakaloliona kutoka kwa timu yao.
Kwa upande wake beki wa Yanga SC, Mohamed Hussein amesema wachezaji wako tayari kupambana kuhakikisha wanaitetea Ngao ya Jamii.
Ni maandalizi kuelekea game ya Ngao ya Jamii , Yanga vs Simba Agosti 12 LIVE #AzamSports1HD
#NgaoYaJamii2026 #KariakooDerby #YangaSimba
- Title
- SIMBA DAY 2026 | Mtangazaji Peter Otai alivyotangaza goli la Kenya Police kwa Kiingereza
- Runtime
- 1:59
- Date posted
- 21 days ago
- Description
- SIMBA DAY: Msikie mtangazaji @peterotai akilisherehesha goli la Elvis Rupia kwa lugha ya Kiingereza kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba SC..
FT: Simba SC 0-1 Police Kenya
Ilikuwa LIVE #AzamSports1HD
#SimbaDay #SimbaSC #Miaka90 #MechiYaKirafiki #SimbaSC #KenyaPolice
- Title
- VIWANJANI| Mjadala matamasha ya Simba, Yanga yafana, Kariakoo Dabi kutimua vumbi Agosti 12, 2026
- Runtime
- 1:23:08
- Date posted
- 21 days ago
- Description
- Mchambuzi wa soka @michaelhyera_ anaeleza mtazamo wake kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC.
Hyera anaamini nyota waliokuwepo kwenye vikosi vya msimu uliopita wanaweza kupata nafasi zaidi katika mchezo huo kutokana na uzoefu na viwango walivyoonesha msimu uliopita.
Azam TV
- Title
- YANGA DAY 2026 | Peter Otai alivyotangaza magoli yote matatu kwa Kiingreza
- Runtime
- 4:48
- Date posted
- 21 days ago
- Description
- YANGA DAY: Msikie mtangazaji Peter Otai alivyoyasherehesha magoli yote matatu yaliyofungwa kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Yanga SC dhidi ya Aigles du Congo.
Goli la Yanga limefungwa na Peter Shalulile huku magoli mawili ya Aigles du Congo yakifungwa na Talasi Tonny.
#YangaDay #YangaSC #MwakaniTena #Wananchi #MechiYaKirafiki #YangaSC #AiglesduCongo
- Title
- TFF yatoa mfumo mpya wa ununuzi wa tiketi za Ngao ya Jamii, "Tiketi za sasahivi zitakuwa na majina.
- Runtime
- 17:07
- Date posted
- 21 days ago
- Description
- Afisa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo amezungumzia uwepo wa mfumo mpya wa ununuzi wa tiketi kuelekea mchezo wa #NgaoYaJamii na kuongeza kuwa mfumo huo utaanza kutumika leo kuanzia saa nane mchana.
Ndimbo anasema mfumo huo ambao ni rahisi kuutumia unatoa fursa ya kununua tiketi nne kwa mtu mmoja.
Azam TV
- Title
- Yanga SC 1-2 Aigles du Congo | Highlights | Yanga Day 2026 - 09/08/2026
- Runtime
- 14:11
- Date posted
- 21 days ago
- Description
- YANGA DAY: Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Yanga SC dhidi ya Aigles du Congo.
Goli la Yanga limefungwa na Peter Shalulile na magoli ya Aigles du Congo yamefungwa na Talasy Tonny.
FT: Yanga SC 1-2 Aigles du Congo
#YangaDay #YangaSC #MwakaniTena #Wananchi #MechiYaKirafiki #YangaSC #AiglesduCongo
- Title
- YANGA DAY 2026 | Kamwe atia utani baada ya Yanga kufungwa na Aigles du Congo
- Runtime
- 3:27
- Date posted
- 21 days ago
- Description
- YANGA DAY: “Tumewaalika tucheze mechi ya kirafiki, wanaanza kubadilika ndani”
Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe akitia utani baada ya kupoteza kwa magoli 2-1 mbele ya Aigles du Congo.
Akabidhiwa picha iliyochorwa kwa dakika 10.
FT: Yanga SC 1-2 Aigles du Congo
#YangaDay #YangaSC #MwakaniTena #Wananchi #MechiYaKirafiki #YangaSC #AiglesduCongo
- Title
- YANGA DAY 2026 | Neno la makocha wa timu zote mbili baada ya mechi
- Runtime
- 5:46
- Date posted
- 21 days ago
- Description
- YANGA DAY: Neno kutoka kwa makocha wa timu zote mbili wakizungumza baada ya mechi kumalizika.
Ni Manqoba Mngqithi wa Yanga SC na Bruno Ferry wa Aigles du Congo.
FT: Yanga SC 1-2 Aigles du Congo
Ilikuwa LIVE #AzamSports1HD
#YangaDay #YangaSC #MwakaniTena #Wananchi #MechiYaKirafiki #YangaSC #AiglesduCongo
- Title
- Yanga SC 1-2 Aigles du Congo | Magoli | Yanga Day 2026 - 09/08/2026
- Runtime
- 4:31
- Date posted
- 21 days ago
- Description
- YANGA DAY: Tazama magoli yote matatu yaliyofungwa kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Yanga SC dhidi ya Aigles du Congo.
Goli la Yanga limefungwa na Peter Shalulile na magoli ya Aigles du Congo yamefungwa na Talasy Tonny.
FT: Yanga SC 1-2 Aigles du Congo.
#YangaDay #YangaSC #MwakaniTena #Wananchi #MechiYaKirafiki #YangaSC #AiglesduCongo
- Title
- YANGA DAY 2026 | Udambwidambwi wa Yanga baada ya kuzimwa taa
- Runtime
- 5:04
- Date posted
- 22 days ago
- Description
- YANGA DAY: Tazama udambwidambwi wa Yanga baada ya kuzima taa.
#YangaDay #YangaSC #MwakaniTena #Wananchi #MechiYaKirafiki #YangaSC #AiglesduCongo
- Title
- YANGA DAY 2026 | Mohamed Mmachinga asema rekodi yake kazi kuivunja
- Runtime
- 1:23
- Date posted
- 22 days ago
- Description
- YANGA DAY: Mkongwe wa Yanga SC, Mohamed Hussein Mmachinga asema rekodi yake ya kufunga magoli 26 kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, yaweza kuwa mbinde kuivunja.
Mchezaji huyo aliiweka rekodi hiyo mwaka 1996.
Ni shamrashamra za tamasha la #YangaDay
#YangaDay #YangaSC #MwakaniTena #Wananchi
- Title
- YANGA DAY 2026 | Shabiki wa Yanga aifuata timu yake kutokea Katoro
- Runtime
- 1:45
- Date posted
- 22 days ago
- Description
- YANGA DAY: Shabiki wa Yanga SC, Jumanne Misungwi asema ametoka Katoro Geita kuifuata timu yake katika dimba la Uhuru huku akitoa ushauri kwa watani wao.
Ni shamrashamra za tamasha la #YangaDay
#YangaDay #YangaSC #MwakaniTena #Wananchi
- Title
- YANGA DAY 2026 | Msigwa akoshwa na Yanga walivyoupamba dimba la Uhuru
- Runtime
- 3:29
- Date posted
- 22 days ago
- Description
- YANGA DAY: Katibu Mkuu wa Wizara Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa aonesha kukoshwa na namna Yanga imeupamba Uwanja wa Uhuru leo.
Ni shamrashamra za tamasha la #YangaDay
#YangaDay #YangaSC #MwakaniTena #Wananchi
- Title
- SIMBA DAY 2026 | Simba SC 0-1 Kenya Police | Highlights - 08/08/2026
- Runtime
- 10:53
- Date posted
- 22 days ago
- Description
- SIMBA DAY: Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mechi ya kirafiki kati ya Simba SC dhidi ya Kenya Police
Goli limefungwa na Elvis Rupia.
FT: Simba SC 0-1 Police Kenya
#SimbaDay #SimbaSC #Miaka90 #MechiYaKirafiki #SimbaSC #KenyaPolice
- Title
- SIMBA DAY 2026 | Goli Elvis Rupia akiifunga Simba kwenye tamasha lao
- Runtime
- 1:56
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- SIMBA DAY: Hii hapa ‘chuma’ ya Elvis Rupia akifunga goli pekee kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba SC.
FT: Simba SC 0-1 Police Kenya
#SimbaDay #SimbaSC #Miaka90 #MechiYaKirafiki #SimbaSC #KenyaPolice
- Title
- SIMBA DAY | Hotuba yote ya Mohamed Dewji kwenye tamasha la Simba
- Runtime
- 15:04
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- SIMBA DAY: “Lazima tufike fainali na kuletea kombe la Afrika nyumbani”
Mwekezaji wa Simba na Rais wa Heshima, Mohamed Dewji anasema ili kufikia ndoto ya kuleta taji la Afrika nchini, ni lazima kuwekeza kwenye miundombinu ikiwemo kujenga kiwanja cha kuchezea mechi za ndani.
#SimbaDay #SimbaSC #Miaka90 #MechiYaKirafiki #SimbaSC #KenyaPolice
- Title
- SIMBA DAY 2026 | Mo Dewji asema usajili bado haujaisha
- Runtime
- 1:14
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- SIMBA DAY: “Hela zipo benki”
Mwekezaji wa Simba na Rais wa heshima Mohamed Dewji anasema usajili bado haujaisha na mzigo wa fedha upo benki.
Ni shamrashamra za #SimbaDay
#SimbaDay #SimbaSC #Miaka90
- Title
- SIMBA DAY 2026 | Golikipa Yakubu Selemani atambulishwa Uhuru
- Runtime
- 1:44
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- SIMBA DAY: Golikipa Yakubu Selemani atambulishwa ndani ya dimba la Uhuru.
Ni shamrashamra za #SimbaDay
#SimbaDay #SimbaSC #Miaka90
- Title
- SIMBA DAY 2026 | Ahmed Ally aingia na Simba wawili wa porini
- Runtime
- 3:45
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- SIMBA DAY: Eba hii kali…Semaji Ahmed Ally aingia na simba wawili wa porini…Kila mtu abaki mdomo wazi.
Neno moja tu kwa semaji
Ni shamrashamra za #SimbaDay
#SimbaDay #SimbaSC #Miaka90
- Title
- SIMBA DAY 2026 | Mangungu asema Simba ndio timu ya kwanza kuwa na jengo lake
- Runtime
- 5:38
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- SIMBA DAY: Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu anasema ni timu ya pili kuwa na nyumba yake yenyewe baada ya Cosmo Politan,
Ni shamrashamra za #SimbaDay
#SimbaDay #SimbaSC #Miaka90
- Title
- SIMBA DAY 2026 | Kagere aishauri Simba ichukue Ligi ya Mabingwa Afrika
- Runtime
- 2:58
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- SIMBA DAY: “Wachukue hata Champions League”
Nyota wa zamani wa Simba SC, Medie Kagere ameishauri ichukue makombe zaidi kwa sababu ni timu kubwa,
Ni shamrashamra za #SimbaDay
#SimbaDay #SimbaSC #Miaka90
- Title
- SIMBA DAY 2026 | Okwi akumbushia ushindi wa magoli matano dhidi ya Yanga
- Runtime
- 3:04
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- SIMBA DAY: Nyota wa zamani wa Simba SC, Mganda Emmanuel Okwi azikumbuka nyakati ambazo walipata ushindi wa magoli matano dhidi ya Yanga.
Afunguka sababu za kutopiga penati siku hiyo ambayo ingemfanya aifikie rekodi ya mkongwe Abdallah Kibadeni ya kufunga hat trick.
Ni shamrashamra za #SimbaDay
#SimbaDay #SimbaSC #Miaka90
- Title
- SIMBA DAY 2026 | Nyota wa zamani Simba SC, Aman Simba afunguka jina lake lilivyomponza
- Runtime
- 3:35
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- SIMBA DAY: Mchezaji wa zamani wa Simba SC, Amani Simba amefunguka namna alivyokosa ‘ulaji’ Yanga kisa jina lake.
Mwenyewe adai kwamba fursa ya kujiunga na Yanga ilikuja mapema zaidi kuliko Simba.
Ni shamrashamra za #SimbaDay
#SimbaDay #SimbaSC #Miaka90
- Title
- SIMBA DAY 2026 | Emmanuel Gabriel asubiri kwa hamu Simba Day ya mwaka huu
- Runtime
- 1:08
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- SIMBA DAY: Nyota wa zamani wa Simba SC, Emmanuel Gabriel anasema anasubiri kwa hamu kuona tamasha la Simba Day litakavyokuwa mwaka huu kwasababu la mwaka jana lilifunika sana.
Ni shamrashamra za #SimbaDay
#SimbaDay #SimbaSC #Miaka90
- Title
- SIMBA DAY 2026 | Shabiki adai kutoroka hospitali akiiwahi Simba Day
- Runtime
- 1:41
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- SIMBA DAY: Kuna mwamba huyo kutoka Mtwara, adai kutoroka hospitali kwa ajili ya sherehe za #SimbaDay.
Mtazame mwenyewe namna alivyo
Ni shamrashamra za #SimbaDay
#SimbaDay #SimbaSC #Miaka90
- Title
- SIMBA DAY | Shabiki wa Simba aimba wimbo wa miaka 90 ya mnyama
- Runtime
- 8:47
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- Zisikie tambo za mashabiki wa Simba SC ambao wamejitokeza mapema leo katika dimba la Uhuru.
- Title
- Rayon Sports FC 2-1 Gor Mahia FC| Final Highlights | CECAFA Kagame Cup 2026 - 07/08/2026
- Runtime
- 15:54
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- Azam TV
- Title
- Jamus FC 1-2 Al Hilal SC | Highlights | CECAFA Kagame Cup 2026 - 07/08/2026
- Runtime
- 8:21
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- Azam TV
- Title
- ZAWADI ZA WASHINDI WA CECAFA KAGAME CUP 2026 | 07/08/2026
- Runtime
- 4:43
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- -Bingwa amepata Dola 30,000 sawa na Shilingi za Kitanzania Milioni 79,411,996.
-Mshindi wa pili amepata Dola 20,000 sawa na Shilingi za Kitanzania Milioni 52,933,761.
-Mshindi wa tatu amepata Dola 10,000 sawa na Shilingi za Kitanzania Milioni 26,466,880.
- Title
- NA HAWA NDIO MABINGWA WA CECAFA KAGAME CUP 2026 | RAYON SPORTS FC | 07/08/2026
- Runtime
- 3:16
- Date posted
- 23 days ago
- Description
- Azam TV
- Title
- Rayon Sports 2-1 Gor Mahia FC | Magoli | CECAFA Kagame Cup 2026 - 07/08/2026
- Runtime
- 4:35
- Date posted
- 24 days ago
- Description
- Azam TV
- Title
- Jamus SC 1-2 Al Hilal SC | Magoli | CECAFA Kagame Cup 2026 - 07/08/2026
- Runtime
- 3:41
- Date posted
- 24 days ago
- Description
- Azam TV
- Title
- Simba SC Agosti 8, Yanga SC Agosti 9 | Uchambuzi wa vikosi, wachezaji na msimu mpya.
- Runtime
- 1:28:43
- Date posted
- 24 days ago
- Description
- "Ni sikukuu kwa Simba na wadau wa mpira wa miguu," amesema mchambuzi wa soka @ramadhani_mbwaduke akizungumzia Simba Day ya 17 ya Klabu ya Simba SC inayotarajiwa kufanyika kesho Agosti 8, 2026.
Mbwaduke amesema kesho ndiyo siku ambayo wanachama, wapenzi na mashabiki wa Simba SC wataona rasmi timu yao ikiwa katika kikosi kamili kitakachoitumikia klabu hiyo kwa msimu wa 2026/2027.
Azam TV
- Title
- ZILIZOBAMBA MITANDAONI: Simba ,Yanga na Azam zatamba na uzi mpya.
- Runtime
- 12:59
- Date posted
- 24 days ago
- Description
- Azam TV
- Title
- SIMBA PRESS: “Biashara kamili itaanza wiki ijayo” | kauli ya Steve Barker kuelekea ya Simba Day.
- Runtime
- 16:32
- Date posted
- 24 days ago
- Description
- Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya Polisi FC ya Kenya utakaochezwa kwenye Simba Day.
Barker amesema Simba Day ni fursa ya timu kujumuika na mashabiki wake kabla ya kuanza rasmi kwa msimu mpya huku akisisitiza kuwa ushindani wa kweli utaanza wiki ijayo.
Kwa upande wa mchezaji wa timu hiyo, David Kameta (Duchu) amesema wachezaji wamepata muda mzuri katika maandalizi ya msimu mpya; na kuwa kesho wataonesha burudani kutokana na kile walichokipata katika kipindi hicho cha maandalizi.
#SimbaDay #SimbaSC #KenyaPolisiFC
- Title
- Simba SC TV | Wiki hii imeangazia matukio katika siku ya uzinduzi wa wiki ya Simba Day na jezi mpya.
- Runtime
- 24:07
- Date posted
- 24 days ago
- Description
- Azam TV
- Title
- ZILIZOBAMBA MITANDAONI | Ahmed Ally atangaza namna atakavyoingia Simba Day, Yanga yazindua jezi
- Runtime
- 24:28
- Date posted
- 25 days ago
- Description
- Azam TV
- Title
- UCHAMBUZI: Kwa nini Djigui Diarra ndiye golikipa bora wa Ligi Kuu Tanzania.
- Runtime
- 1:44:15
- Date posted
- 25 days ago
- Description
- Mchambuzi wa soka, Godlisten Muro akizungumzia umuhimu wa nafasi ya golikipa katika mafanikio ya klabu, amesema kuwa uti wa mgongo wa timu huanzia kwenye safu ya ulinzi ambayo msingi wake mkuu ni golikipa akishirikiana kwa karibu na mabeki.
Muro ameeleza kuwa uimara wa golikipa wa Yanga SC, Djigui Diarra amefanikiwa kuipa timu hiyo utulivu wa kujenga matokeo mazuri ambayo yameongeza nafasi ya klabu hiyo kutwaa mataji mara tano mfululizo.
Kwa upande wake mchambuzi wa soka Deotraphe Kiungai anaamini kuwa wachezaji wanapaswa kuhukumiwa kulingana na majukumu yao uwanjani.
Deo amesema wachezaji wakitimiza majukumu yao ipasavyo uwanjani, timu inapata uwiano mzuri wa utendaji uwanjani ambao huipa nafasi kubwa klabu ya kushindania na hatimaye kutwaa ubingwa.
Azam TV

